Kajiru

Ushuhuda (S.M.)

  Tafadhali kumbuka kuwa kabla sijasimulia kile kilichoonekana kutokea katika miezi michache iliyopita, kusimulia huku ni tafsiri ya matukio kulingana na ufafanuzi wa kiakili na taswira, kuanzia sasa tukitazama nyuma kwa uwazi kwamba hakuna maneno yanayoweza kugusa jinsi tulivyo. Hali ya kiroho ilikuwa chanzo cha msukumo, mwishilio na uboreshaji kwa kile nilichofikiria kuwa ni mimi kabla ya Machi 2022. Ilikuwa… Read more →

Asili na Kuzaliwa Upya “Essences and Reincarnation”

  Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita tumepokea taarifa kutoka kwa Uongozi wa Kiroho kuhusu Ngazi za juu za Maumbile ambazo tutaishi baada ya kifo chetu cha kimwili. Zaidi ya hayo, tumepewa Maarifa kutoka kwa marafiki na jamaa ambao wamevuka hadi katika Ulimwengu wa Mbinguni. Inaonekana, kila mmoja wetu Anatoka kwa Kiini ambacho kinakaa katika Ngazi za juu za Kiroho.… Read more →

Kutabiri Yajayo

  Watu siku zote wamekuwa wakitaka kujua siku zijazo zinaweza kuleta nini, kwa hivyo kuwa na nia na hamu ya Clairvoyance, Astrology, Tarot, Runes na I Ching nk. Uelewa wa kweli wa utabiri hutegemea swali moja: Je, sisi binadamu tunao Uhuru wa Kutaka au “Free Will”? Ikiwa jibu ni hapana, basi kila kitu katika maisha yetu lazima kiwe kimepangwa mapema… Read more →

Maana ya Ukombozi Wa Ufahamu au “Enlightenment”

  Maana ya Ukombozi Wa Ufahamu au “Enlightenment” ni Hali ya Kuwa. Anapopata Ukombozi Wa Ufahamu au “Enlightenment” Mtafutaji huvuka Ngazi zote za Ufahamu na kuunganishwa na Umoja unaoenea katika Uumbaji wote. Katika Umoja: Hakuna Mwanga. Hakuna Sauti. Hakuna wakati. Hakuna kushoto, kulia, juu, chini, mbele au nyuma. Hakuna maumbo, sura au rangi. Hakuna mipaka. Muhimu zaidi hakuna wewe! Ukombozi… Read more →

Kujiponya

  Hili limetoka kwa Samuel* kwa wale wanaotaka kujiponya. Njia rahisi, fupi kwa mtu yeyote kufanya mazoezi, katika umri wowote, na hauhitaji ujuzi wowote. Kama vile unavyoweza kufanya mazoezi, kila siku, kuleta Mwanga na Upendo katika maisha yako unaweza pia kuleta uponyaji. Ni kidogo sana kinachoeleweka kuhusu mwili wa mwanadamu; kuna mambo mengi sana yanayotokea ndani ya kila mtu ambayo… Read more →

Afya

  Kuishi katika Ulimwengu wa teknolojia hakutakuwa rahisi – ingawa kumekuwa na maendeleo ya kushangaza katika uponyaji na mawasiliano, hasara na matatizo ni wazi kuonekana. Inashangaza sana kupata data inayokuambia ni kiasi gani watu wanatumia simu zao za mikona na kompyuta kila siku! Nishati ya microwave inayotumiwa katika vifaa hivi inasababisha matatizo ya afya, bila kuzingatia kutofanya kazi wakati wa… Read more →

Ushuhuda (E.H.)

  Habari wote (Aprili 2022), Nilianza kutahajudi kwenye Mwanga na Sauti ya ndani tarehe 12 Septemba mwaka jana. Kabla ya Kuanzishwa nilifanya tahajudi ya mantra. Wakati huo nilikuwa tayari naona Mwanga mwingi. Hata hivyo akili ilikuwa ikiniongoza wakati huo kwa nilichokiona. Jiometri ilikuwa tofauti. Niliona majengo mengi na kila aina ya asili. Baada ya Kuanzishwa nalinganisha kutahajudi kwangu na Yin… Read more →

Picha Kubwa kwa Ujumla

  Kichwa cha Habari cha tovuti yetu kinapendekeza kwamba sisi ni Kikundi cha Kutahajudi. Hii bila shaka ni kweli, lakini inafurahisha kutambua kwamba Mawasiliano ya kwanza kutoka kwa Utawala wa Kiroho, mwishoni mwa mwaka 2014, yalikuwa kuhusu aina pekee mpya za Nishati na Ulimwengu. Tuliongozwa kutengeneza mashine maridadi kwa kutumia teknolojia ya koili mbili ambayo inaweza kuonyeshwa kubadilisha ufahamu wa… Read more →

Ushuhuda (I.N.)

  Ilikuwa usiku wa tarehe 28 Disemba 2021, tukiwa katika zoezi la kutahajudi, mwalimu wetu aliyekuwa akituongoza alikuja na kunigusa. Niliona mwanga Mweupe, ambao baadaye ulififia na kisha likaja ua hili kubwa la zambarau lililochanua. Kesho yake tuliendelea na tafakari, siku hii nilianza kusikia sauti za vitu, baadaye nikawa nasikia sauti kama mawimbi ya maji ya mto unaotiririka, na sauti… Read more →

Ufahamu

  Kama wanadamu tunajiona kuwa tuna ufahamu. Ufahamu wetu unategemea pembejeo kutoka kwa hisia zetu tano, hisia zetu na mawazo. Tunaweza kuona wazi kwamba wanyama pia wana ufahamu kwa jinsi wanavyoitikia kutokana na uchochezi wa mazingira. Ingawa sayansi inaweza kuwa na mpaka kuhusu ufahamu wakati tunapozingatia ufalme wa mimea. Mimea pia huguswa na mazingira yao lakini je, hiyo ni sawa… Read more →