Dunia Nzima

 
Kuelekea mwishoni wa mwaka 2014 tulipokea habari kutoka kwa Uongozi wa Kiroho juu ya muunganiko wa Ajabu ambao upo kati ya Sayari yetu na vitu vingine kwenye ulimwengu.

Iliwasilishwa kwa ishara, kana kwamba duniani tunakaa chini ya msingi wa almasi kamili na tumeunganishwa na kila moja ya sura zake nyingi za alimasi.

Tuliambiwa kuwa ukosefu wa usawa wa Nguvu kwenye sayari yetu ilikuwa na matokeo mabaya yanayofika mbali sana. Ndio sababu ilikuwa muhimu sana kuongeza Ufahamu wa idadi kubwa ya watu kwa wakati huu.

 

 

Tahajudi Ya Dunia Nzima

Tunapenda kukualika kutahajudi pamoja nasi saa 20:00 GMT kila Jumamosi na kutuma Upendo na Mwanga Duniani. Wanadamu wote wana uwezo wa kuelekeza Nguvu za Kiroho na kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko makubwa. Tafadhali elewa kuwa, sio lazima uwe mshiriki wa kikundi chetu; ukiwa mtu tu anayejali kiasi cha kutosha na uko tayari kuikubali hali halisi.

Kama sehemu ya hatua ya jumla kuelekea kuwajali wengine tunapenda kwa kawaida Tahajudi zifanywe kila wiki. Kwa nyinyi nyote kuungana pamoja kwa dakika 10 kwa wakati mmoja. Hii inaweza kuwa taarifa ya nguvu kutoka kwenu kuthibitisha ukubali wenu kwa sayari kwa ujumla. Kwa kufanya hivyo mtahisi muunganiko mkubwa na uhusiano mzuri kwa kila mmoja wenu.


Ili kujua muda huu wa tahajudi kwenye sehemu yako ya Dunia unaweza tu ku“Google”: 20:00 GMT (kwa mfano) Calgary. Kuwa mwangalifu kama unapokaa kuna ya mabadiliko ya wakati wa msimu wa joto au “Summertime”.

 

Ascension

Neno hili linatumiwa mara nyingi zaidi, siku hizi, kuelezea aina fulani ya mpito wa Kiroho. Watu wengi wanatarajia Mungu kuingilia ili kusuluhisha matatizo ya Sayari yetu dhaifu. Hatuoni hii kama janga la mara moja, lakini kama mchakato taratibu ambao unafanyika hivi sasa. Idadi kubwa ya watu wanapata Uamsho bila kutegemea na kwa hiari wanabadilisha jinsi wanayoishi na kuiona dunia. Wengine huhisi kulazimika kutafuta Mwanga na Sauti kwa kupitia Tahajudi.


Watu kote duniani wanagundua tuko katika wakati muhimu katika mabadiliko na ukuaji wetu kama binadamu na ikiwa tutakwepa janga hili tunahitaji kuchukua hatua sasa!