Asili na Kuzaliwa Upya “Essences and Reincarnation”

 

Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita tumepokea taarifa kutoka kwa Uongozi wa Kiroho kuhusu Ngazi za juu za Maumbile ambazo tutaishi baada ya kifo chetu cha kimwili. Zaidi ya hayo, tumepewa Maarifa kutoka kwa marafiki na jamaa ambao wamevuka hadi katika Ulimwengu wa Mbinguni.

Inaonekana, kila mmoja wetu Anatoka kwa Kiini ambacho kinakaa katika Ngazi za juu za Kiroho. Tunaweza kutumia neno Nafsi kuwakilisha Nishati inayohuisha mwili wetu na kushuhudia hisia na akili zetu. Nafsi iko hapa ili kujifunza masomo ambayo yalifanyiwa kazi kwa uangalifu kabla ya kuzaliwa kwetu na kurudisha uzoefu wake wa Kidunia ili kuelimisha Kiini.

Kila Nafsi, na kwa hivyo kila umwilisho au mwili au seti ya miili, ni wa kipekee. Njia sahihi zaidi ya kuelewa Kuzaliwa Upya sio kutoka kwa maoni ya mtu binafsi. Kusema kwa mfano, “Niliishi hapo awali” kunapendekeza kudumu kwa Nafsi. Kielelezo bora kitakuwa kusema kwamba Nafsi nyingi zinaundwa na Kiini kimoja. Kwa hivyo ikiwa mtu amerudishwa nyuma “regressed” ana uwezekano mkubwa wa kuangalia kwa ufupi maisha mengine kutoka kwenye Kiini chake.

Inawezekana kabisa kwamba idadi fulani ya Nafsi kutoka kwenye Kiini kimoja inaweza kupata miili au ku“incarnate” kwa wakati mmoja. Wana uwezekano wa kuwa wanafamilia, marafiki wa karibu, wafanyakazi wenza au “partners”. Iwapo mtu ana maisha ya Kiroho na amefikia hali ya juu ya Ufahamu, hakika hii itaboresha na kuinua Kiini chao.

Mtu anapokufa, mwanzoni, ni mwili wa nyama tu ndio unaovukwa “transcended”. Hisia na mawazo yanabaki na yanawajibika kwa ufahamu wetu wa awali wa Ulimwengu wa Kiroho. Hii inathibitishwa na watu ambao wamepata uzoefu karibu na kifo; kimsingi unaunda Mbingu yako mwenyewe!

Wakati huu kuna mapitio ya maisha ambapo unaweza kupata ‘kuona’ mambo ambayo umekosa au kushindwa kujifunza kutoka kwenye maisha yako. Hakuna hukumu, ni ufunuo mpole tu wa kusaidia ufahamu wako. Hatimaye ni wakati wa kuendelea. Katika hatua hii nguvu za kihemko na kiakili huanza kuyeyuka ambayo huruhusu Nafsi kuungana tena na Kiini chake.

Tunajua kutokana na Tahajudi yetu kwamba kwa kiwango fulani Kila Kitu Kimeunganishwa; kwa hivyo haishangazi kugundua kuwa Viini au (Essences) pia huingiliana. Nafsi kutoka kwa Kiini kimoja zinaweza kuchagua kupata mwili na zile za Kiini kingine mara kwa mara, ili kuanzisha ushirikiano kama vile ndoa. Tena, huu ni ugunduzi wa kawaida wakati watu wamerudishwa nyuma “regressed”.

Kama ilivyo kwa uzao wa familia “family trees”, ukirudi nyuma vya kutosha, kila mtu ana uhusiano! Tunadhani hii pia ndivyo ilivyo kwa Viini au “Essences”, kwamba zote zitatoka kwa Monad ya moja ya Binadamu – jambo la kufikiria!

Tuliyoandika yasichukuliwe kuwa ya uhakika wa mwisho; ni kielelezo rahisi tu cha kutusaidia kupata ufahamu fulani wa somo. Kadri tunavyokusanya maelezo zaidi ni lazima kwamba kielelezo kitahitaji kusasishwa.