Kuanzishwa

 
“Wakati nilipokaa kutahajudi kwenye kikao cha kuazishwa kwa kweli sikuwa natarajia mengi. Watu huwa wanazidisha na kukuza mambo lakini kwa kawaida ni kwa sababu ya shauku na sio udanganyifu. Kwa hivyo nilikuwa na uwazi wa akili niliapoamua kukaa kwenye mto wangu siku hiyo.

Kwa jinsi yoyote ile nisingeweza kuwa tayari kwa kile kilichotokea wakati nilipopewa Cheche ya Mungu (Divine Spark); Nilihisi kana kwamba nilikuwa nikirushwa kwenye anga na kupita galaxies za nuru nzuri kabisa isiyoweza kufikirika, za rangi nyeupe na dhahabu. Nilichotaka kufanya wakati huo ni kufa hapo hapo, kwa kugundua kuwa ingawa nilijiona kuwa nina elimu, sikujua chochote.

Ni wazi nilirudi kutahajudi tena siku nyingine. Miaka kadhaa baadaye nilipata Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho (Enlightenment) na sasa niko kwenye nafasi ya kusaidia wengine kwenye Njia hiyo hiyo.”
 

Utangulizi

Kuanzishwa (Initiation) tunayoongelea imefanyika katita karne na miaka yote na imetajwa katika vitabu vya Kiroho kama vile Bibilia na Bhagavad Gita.
Hadithi ya bibilia ya Yohana Mbatizaji na Yesu inapendekeza kabisa kwamba Yohana alitoa ufunuo wa Nishati ya Mwanga na Sauti ambazo zilitajwa kama Njiwa Mtakatifu. Kwenye Bhagavad kuna maelezo ya ajabu ya Bwana Krishna akifunua Umbo lake la Kiungu (Divine Form) kwa Arjuna.

 

Mwanga na Sauti

Mtafutaji anaunganishwa na Nishati za Ngazi za Kiroho kwa Kuanzishwa (Initiation) kwenye Nuru na Sauti. Ingawa tunatumia maneno yale yale, haya hayatakiwi kuchanganywa na yale ya kimwili; Nguvu hizi hazigunduliki kupitia akili na hisia za chini. Hasa Mwanga unaweza kuwa na Ubora usioelezeka na Mwangaza mkali na unaonekana kuwa hai. Watahajudi wanaripoti kuhisi Upendo mkubwa na Furaha wakati wa kuungana na Mwanga huu.
Hata baada ya kupata maajabu ya kushangaza ya Nguvu hizi haiwezekani kuzifahamu kiakili. Sio matokeo ya kujitakia au matokeo ya mawazo ya kutamani na mawazo ya kupita kiasi.
Ujuzi wa Kweli wa Kiroho wakati wote unafunuliwa; haupatikani kamwe katika vitabu!
 

Uhamisho

Kuanzishwa (Initiation) kwenyewe kunafanyika kwa mguso mwepesi kichwani na Mwalimu ambaye amepata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment(vinginevyo, Uhamisho wa Nishati unaweza kufanywa kwa mbali “remotely”). Utaratibu na mchakato huu unaunda na kumuunganisha Mtahajudi kwenye Ngazi za juu za Ufahamu wa Kiroho.

Kwa uelewa wetu Chanzo cha Nguvu ni Viumbe wa Kiroho au (Intelligence) tunaowaita Uongozi wa Kiroho. Wanawaongoza Walimu wetu ambao huwa kama mfereji tu wa kupitisha nguvu hizi.

Mtu anapoanzishwa kuna wigo mzima wa uwezekano, toka kuwa “subtle” hadi kupita akili kabisa.

 

Njia

Baada ya Initiation au Kuanzishwa, kuna Njia ya ndani ambayo inaweza kufuatwa, ambayo hatimaye inaongoza kwenye Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment. Ingawa unaweza kupokea mafundisho ya kukusaidia njiani, Nishati hizi za Mwanga na Sauti ndio Viongozi wako wakati unapokaa kwenye kikao cha Tahajudi. Sauti itakuongoza katita Upanukaji wako na Mwanga utakufundisha kile unachohitaji kujifunza.
Ni kama vile ni Walimu kamili, kwa hivyo, watangojea mpaka mwanafunzi anapokuwa tayari. Hauwezi kudhibiti Tahajudi zako na akili yako inaweza kuzuia Mwanga na Sauti bila kujua. Kinachohitajika ni kujiachia, kuachilia na uaminifu. Hii inasikika kama rahisi, lakini kwa ujumla inahitaji kujitolea, uvumilivu na mazoezi.
Watahajudi wote huwa wanasema kwamba wakati walipokuwa na maendeleo kwa ujumla ilikuwa wakati ambao hawakutarajia. Watu mara nyingi huripoti kwamba Nguvu za Kiroho kwa namna fulani ziliwashikilia na kuwatembeza kwenye Njia ya Kiroho.
 

Maandalizi

Tunawaambia watu wachukue mtindo wa maisha mzuri ambao unajumuisha hali zao za kiafya, kimwili, kihisia na kiakili. Unajua kinachofanya kazi vizuri kwako na inabakia kuwa jukumu lako.

Kabla hatujaanzisha mtu tunataka kuhakikisha kuwa yuko makini na anataka kuunganishwa na Mwanga na Sauti na ameelewa kile anachoomba. Tutatoa mwongozo katika tahajudi rahisi ya pumzi na pia kutoa Mantra kuleta usawa na uwiano, kuzingatia na kujiachia.

Baada ya kukuanzisha, tunachukua jukumu letu kwa umakini sana kwa hivyo tunatambua umuhimu wa kukupa msaada wakati wa safari yako kwenye Njia yako. Kwa bahati nzuri, wale ambao hufanya zoezi hili la kutahajudi wako tayari kuongoza na kusaidia wengine. Kulingana na mazingira na eneo lako la kijiografia, hii inaweza kwa kawaida kuwa mikutano ya uso kwa uso, mawasiliano ya simu, mtandao na media za kijamii au majukwaa ya mawasiliano ya video. Hakuna vikwazo na hakuna chochote kinachodaiwa kwako. Kama ilivyoelezwa hapo awali, tunakataa michango ya aina yote ile – kila kitu tunachofanya ni bure kabisa!

 
Wasiliana na Walimu wa Kutahajudi