“Nilipokuwa naendesha juu ya kilele cha kilima ufahamu wangu wote na kile nilichohisi ni mimi kililipuka na kuwa kila kitu nilichoweza kuona. Nakumbuka wazi kabisa kuangalia miti, barabara, magari mengine, mashamba na anga… kila kitu kwa upande wake kilikuwa kinatetemeka na mapigo ya aina na mwanga ambao ulifanya kila kitu kionekana kuwa kipya kabisa. Kwa maana hiyo hakukuwa na tofauti yoyote kati ya vitu ambavyo nilivitazama.
Nilianza kucheka mwenyewe kwa sababu niligundua kuwa ingawa nilikuwa kwenye gari inayokewnda kasi barabarani, sikuwa naenda mahali popote. Nilikuwa naenda mbele lakini cha kushangaza na kitendawili cha nguvu hii ambayo ilijaa kote ambapo nilihisi ni mimi, kamwe haikutembea. Kulikuwa na mwanga kutoka kwa vitu hivi vyote na kila kimoja kilionyesha, kile kinachoweza kuelezewa kama, mwanga wa mbinguni.
Uzoefu/uamsho huu ulidumu mchana wote na jioni. Huo ndio ulikuwa udhibitisho ambao nilihitaji kugundua kuwa kulikuwa na kitu zaidi ya kuishi na ufahamu wa wanadamu kuliko vile ambavyo kwa kawaida tunavyoongozwa kuamini.
By the way, ikiwa labda unaweza kushangaa, sikuwa kwenye madawa za kulevya, hata sijawahi kujaribiwa!”
Aina za Uamsho
Watu wengi ambao wameongozwa kwenye tovuti hii tayari wana aina fulani ya Uamsho na wana hamu ya kujifunza zaidi. Uamsho unaweza kutofautiana kutoka maono bila kutegemea na upanukaji, mpaka kwa aina fulani za mazoea ya kutahajudi kama Kundalini.
Uamsho bila kutegemea, kama jina linavyopendekeza, hutokea bila kutegemea au sababu yoyote ya kimantiki. Mtu anaweza kuwa anaendalea na maisha yake ya kila siku, na ghafla wanaweza kupata uzoefu: Sauti ya juu, kuona Mwanga mzuri au kuwa na hisia kubwa za Upendo na Furaha. Watu wengi ambao wanaripoti matukio haya hawajawahi hata kutahajudi, au hata kujiona kama ni watu wa kiroho.
Dalili
Tunaamini watu wengi wakati mmoja au mwingine wanapewa ufahamu wa kile kilicho zaidi ya maisha. Kwa wengine inaweza kuwa hila na laini, kwa wengine inaweza kuwa zaidi ya maelezo yoyote ya kimantiki. Hata hivyo, mara nyingi inamaanisha kwamba mtu hukaa kimya kuhusu Uzoefu wake; wanaona kuwa familia na marafiki watapunguza uzoefu wao kuwa fikira zisizokuwa na msingi au kukosekana kwa usawa wa hisia.
Kama tulivyosema kwenye ukurasa wa Kuanzishwa, Nguvu tunazozisema haziwezi kufikirika, haijalishi tunajaribu sana kwa kiasi gani. Kwa kweli, watu wengi wanasema kuwa Uzoefu, wakati huo, ulionekana kuwa halisi kuliko ukweli wao wa kawaida wa kila siku. Ni kana kwamba akili na hisia zao zote zilikuwa zimeongezeka ghafla!
Chaguo
Baada ya kupata Uamsho kama huu mtu ana chaguo kadhaa:
Wanaweza kukaa kimya bila kusema.
Wanaweza kuwaambia wengine na labda wataandika kuhusu Uamsho wao.
Wanaweza kujaribu kurudi kwenye Ngazi za Kiroho na kuelewa na kutatua fumbo.
Tovuti hii inawakilisha kikundi cha Walimu ambao wamejitolea maisha yao kusaidia watu, wa asili zote, imani na madhehebu, kupata Ukweli. Kwa wale ambao tayari mmepata dalili, basi ni rahisi kwenu kuelewa na kukubali kile tunachotoa.
Tunataka kuwapa mazoezi ya Kutahajudi ambayo yatawaunganisha kwa kudumu na Nguvu hizi. Hii itawapa fursa ya kupitia tena uzoefu wenu na mara nyingi huenda hata zaidi Kusafari na kupata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment.
Uamsho na Njia ya Kiroho
Tunaambiwa kwamba kulikuwa na wakati, maelfu ya miaka iliyopita, wakati ambapo Binadam ilibidi apate hali ya Kiroho peke yake. Hii kawaida ilifanikishwa kwa kujitoa kutoka kwenye jamii na kupata pango au jangwa na kisha kutumia miongo kadhaa kutahajudi.
Baadaye ilizingatiwa kuwa muhimu kwa watu zaidi kupata Hali za Kiroho, ndiyo sababu Njia ya Mwanga na Sauti iliundwa na “Akili” au “Intelligence” tunayoiita kama Uongozi wa Kiroho.
Mfumo huo ulihusisha Mabwana au “Masters” ambao walikuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na Uongozi wa Kiroho. Wangevutia wanafunzi wachache, na ikiwa wanafunzi wataonekana kuwa wanastahili, wangeweza Kuanzishwa. Katika siku za mwanzo ilikuwa nadra kwamba mtu yeyote, mbali na Mwalimu au “Master”, angepata Ukombozi wa Ufahamu au “Enlightenment”.
Mfano mzuri wa hii ni Guru Nanak (1469 – 1539) ambaye ni Baba wa “Sikhism” ambayo ilileta vikundi vya Kutahajudi kama vile Sat Mat.
Tukienda mbele haraka hadi karne ya 20 tunapata “Masters” wengi na Njia nyingi za Kutahajudi ambazo zilidai kukufikisha kwenye “Enlightenment” au Ukombozi wa Ufahamu. Cha kusikitisha ni kuwa, wengi waliharibiwa na ufisadi wa pesa, “ego” au ubinafsi na hamu ya madaraka.
Hii ilisababisha vikundi kama chetu kupewa nafasi ya kupitisha na kutoa Mwanga na Sauti bila Mwalimu, “Master” au kiongozi. Tumeweza pia kufanya kazi vizuri kabisa bila kuhitaji kutoza pesa au kutafuta na kupata majengo. Kwa maana fulani tumekuwa jaribio na kulingana na Uongozi wa Kiroho tumefanikiwa sana!
Walakini, mabadiliko makubwa yamefanyika kwa matokeo ya sisi kufikia lengo letu la kuwa na watu 75,000 Walioanzishwa mpaka kufikia mwaka jana (2020). Idadi kubwa ya watu ulimwenguni kote sasa wanaamka na wana Utambuzi wa Kiroho wa kushangaza. Wengine pia wanajua Nishati ya Mwanga na Sauti.
Wengi wao wanakubali tu kile kilichowapata lakini wengine wana shauku ya kutaka kujua na wanaanza kutafuta kwenye mitandao kupata majibu. Wakati mwingine watataka tu kuhakikishiwa lakini wengi wanataka kupata uzoefu zaidi, na ikiwezekana kupata Ukombozi wa Ufahamu au “Enlightenment”.
Katika mwaka uliopita hivi au zaidi, maswali mengi tunayopata kupitia tovuti ni kutoka kwa watu ambao wamekuwa na aina fulani ya Uamsho. Kile tulichogundua ni kwamba wakati tunawaanzisha hawawezi kuona alama za kawaida ambazo washiriki wetu wa asili walizipata.
Imeelezwa kwetu kwamba wanajiunga kwenye Njia katikati au njiani na sio mwanzoni. Kwa hivyo kwa kawaida watafanya Utambuzi hata bila kufahamu, kwa mfano, lotus la petali 1000. Hii haipunguzi kwa njia yoyote kina na ukubwa wa Utambuzi wao – kilicho muhimu ni Hali ya Ufahamu wa Mtahajudi.
Katika siku za usoni inawezekana kwamba watu wengi walio na Uamsho wa Kiroho wataweza kukamilisha Njia yao ya Kiroho bila kuhitaji Kuanzishwa. Walakini, tuko katika hatua ya mpito ambapo tunahitajika sana kuhakikisha kufanikiwa kwa mchakato wa Kupaa au “Ascension”.
Watu ambao wameamshwa au wana Mwamsho wengi hawapendi kuendelea zaidi. Utapata tu asilimia ndogo ya watu wanaowasiliana nawe.
Kadri mambo yanavyoendelea, hata hivyo, katika maendeleo ya Kupaa au “Ascension”, watu wataanza kuelezea Uzoefu wao zaidi na wasiwe na hofu ya kusikika kuwa wa ajabu.
Video
Tumetengeneza video mbili za Youtube kuwasaidia kuamua ikiwa uzoefu wenu ni wa Kiroho au hisia za mwili tu ambazo zinaendeshwa na akili. Kwa wengi wenu tunagundua kuwa hamna shaka na hatuhitaji mjadala zaidi.
Video ya kwanza inaangalia watu wanaoona Mwanga. Je! Mwanga wa akili au Mwanga wa Ngazi za Kiroho?
Video ya pili inahusika na watu wanaosikia sauti za juu. Mchafuko ambao unajitokeza ni kwa sababu ya hali ya matibabu inayojulikana kama Tinnitus. Kwa hivyo, watu wengi, mara ya kwanza kuisikia Sauti, wanafikiri ni tukio na jambo la mwili.