Analojia Ya Mungu

 
Acha nizungumze kidogo juu ya Mungu.

Mungu anakaa nyuma ya Ulimwengu na wakati huo huo ni Ulimwengu. Nitajaribu kutumia mlinganisho ili kukusaidia kuelewa hili vizuri zaidi.. Fikiri kwamba Mungu ni Bahari ya Maji isiyo na kikomo. Maji kila upande, hakuna mwanzo, hakuna mwisho. Ndani ya maji kunaweza kuwa na mabadiliko ya halijoto na baadhi ya sehemu zinaweza kuwa baridi sana na kutengeneza fuwele za barafu. Fuwele hizo zingekuwa na sura na umbo; zingeonyesha ubinafsi. Hata hivyo, hazingekuwa za kudumu na hatimaye zingeyeyuka na kuunganishwa tena na bahari isiyo na kikomo.

Sisi ni kama fuwele hizo za barafu, tukifikiri tuna ubinafsi. Tunapoutazama Ulimwengu tunaona maumbo na miundo yote. Lakini tunapoanza Kutahajudi tunahisi kwamba kila kitu kimeunganishwa kwa namna fulani….hatuko vile tulivyofikiria. Tunapopata Ukombozi Wa Ufahamu au Enlightenment, kwa muda mfupi tunaungana kabisa na Bahari isiyo na kikomo na kumtambua Mungu…..Nishati inayozunguka na iliyoka kwa Kila kitu. Katika mfano wetu fuwele ya barafu inayeyuka kabisa na kuwa kitu kimoja na Bahari..

Baada ya Ukombozi Wa Ufahamu au Enlightenment tunakuwa fuwele ya barafu tena lakini hatuwezi kamwe kudanganywa kwa kufikiri kwamba tumejitenga kwani tunajua Ukweli: Kila kitu ni Maji (Mungu).

Kwa hiyo, Mwanga na Sauti ni Udhihirisho wa Mungu. Mungu ni zaidi ya Mwanga na zaidi ya Sauti; Mungu ndiye Nishati inayoumba (na wakati huo huo ni) Nishati hizi. Ukisoma Biblia ya Kikristo katika Mwanzo inasema: Mungu alisema, “Kuwe na Mwanga” kwa hiyo Mungu lazima awepo kabla ya Mwanga. Pia inaongelea Neno (Sauti) la Mungu, hivyo tena Mungu alikuwepo kabla ya Neno, kama vile Maji yalivyokuwa kabla ya fuwele ya barafu kudhihirika.


Huu ni mlinganisho rahisi kusaidia kuelezea kisichoeleweka!