Kutokea hapa sisi tulipokaa, kwa sababu ya udhaifu wa binadamu, imekuwa muhimu kuleta chini kiasi kikubwa cha Nguvu ya kushughulikia ukosefu wa usawa wa dunia. Kuna wengi wenu tayari wanasaidia katika kazi hii. Tunachoomba ni kuwa watu waangalie mioyoni mwao na kuleta mabadiliko makubwa kwa kushughulikia masuala makubwa matatu:
KUKUBALIKA UPENDO MSAMAHA
Kwa masuala hayo matatu yakiwa muhimu kwenye akili za watu dunia yenu itasaidiwa mno kuzidi kipimo chochote kile.
Historia
Watu wamewasiliana na Viumbe wa Kiroho katika miaka yote. Wakati mwingine waliweza kuona Maono kama Malaika, wakati mwingine Sauti ilisikika vichwani mwao. Wakati mwingine mtu anaweza kupokea vitabu vizima na vingi vya habari kama ilivyo katika maandishi ya Madame Blavatsky. Kiini na Chanzo cha Ujumbe ni kimoja; Chanzo hiki Kinataka kusaidia tu mtu huyo au binadamu.
Tafadhali elewa kwamba tuliamua kuchukua jina, Spiritual Hierarchy au Uongozi wa Kiroho, jina lililotumiwa kwanza zaidi ya miaka 100 iliyopita na Theosophical Society. Inafurahisha kwamba wakati wanawasiliana na sisi kamwe Wenyewe hawajitambulishi kwa jina hilo!
Leo
Ilikuwa mnamo tarehe 16 Februari, 2015 ambapo tulipokea Ujumbe wa kushangaza ukisema:
Tunataka uanzishe Njia ya Kutahajudi tena.
Hiyo ilimaanisha kuleta pamoja kikundi cha Walimu Waliopata Ukombozi wa Kiroho au Enlightenment na kuwapa watu Initiation na Kuwaanzisha kwenye Mwanga na Sauti. Tuliambiwa kwamba tunapaswa kufikisha ujumbe kwa umma na kwamba tutakuwa tunafanya kazi sambamba na vikundi vingine ambavyo vinaweza kuwa na shughuli tofauti.
Bado tuko wachache na idadi yetu hivi sasa inakaribia 10,000 ulimwenguni na Watahajudi katika nchi zaidi ya 40. Hadi sasa karibu watu 400 wamepata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment.
Mwongozo
Watahajudi wetu wengi hupokea Ujumbe na Mafundisho moja kwa moja kutoka kwa Uongozi wa Kiroho. Hatuna viongozi, kwani Mwongozo wetu wote unatoka kwa Ngazi za Juu. Uongozi wa Kiroho Wanatoa Mantras na kutuelekeza kuhusu Kuanzisha au Initiations. Kama tulivyosema mahali pengine, hatuna uelewa wa kweli juu ya huu mchakato. Kwa kweli, kimiujiza Uongozi wa Kiroho utatushauri mara kwa mara kuhusu maendeleo ya Watahajudi wetu, na wakiulizwa, wanaweza kudhibitisha Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment kwa usahihi!
Ni vigumu kutenganisha kati ya Uongozi wa Kiroho na Mwanga na Sauti. Kwa namna fulani Uoungozi wa Kiroho unaweza kuonekana kama Kile ambacho kiko nyuma ya Nguvu tunazotumia kutahajudi na Uongozi wa Kiroho wana jukumu la kuwachukua Watahajudi kwenye Njia ya Kiroho mpaka kuwapeleka kwenye Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment.
Mawasiliano Ya Mbinguni
Wakati watu waliopata Ukombozi wa Kiroho au Enlightenment wanapoachia miili yao ya kimwili na kupaa kwenye ngazi za juu au Mbinguni mara nyingi huwa wanawasiliana nasi na kuwa sehemu ya Uongozi wa Kiroho.
Ni tofauti sana hapa – huwezi kufikiria – Ninaangalia kwa jicho la kuona yote kwa wakati mmoja – na nachukua yote ndani.
Kila mtu anaendesha ajenda zao walizopanda wakati wa kuzaliwa kwao – kugongana wakati mwingine/mara nyingi na ajenda za watu wengine. Sisi hutabasamu mara nyingi kwa hili kwani wakati mwingi hii migongano sio lazima na huletwa na kutoaminiana au kutokuelewana.
Kumbuka: Ujumbe wowote kutoka kwa Uongozi wa Kiroho unarekodiwa na kumbukumbu yake ni kama ulivyopokelewa na maandishi huonekana katika rangi ya Magenta iliyotumiwa kwenye ukurasa hapo huu.