Kama wanadamu tunajiona kuwa tuna ufahamu. Ufahamu wetu unategemea pembejeo kutoka kwa hisia zetu tano, hisia zetu na mawazo. Tunaweza kuona wazi kwamba wanyama pia wana ufahamu kwa jinsi wanavyoitikia kutokana na uchochezi wa mazingira.
Ingawa sayansi inaweza kuwa na mpaka kuhusu ufahamu wakati tunapozingatia ufalme wa mimea. Mimea pia huguswa na mazingira yao lakini je, hiyo ni sawa na kuwa na ufahamu? Ikiwa tutachukua hatua zaidi na kuangalia ufalme wa madini, hitimisho la wazi litakuwa kwamba haiwezekani kwa vitu visivyo hai kama fuwele (crystals) na miamba kuwa na ufahamu.
Hata hivyo, hitimisho letu huenda likatokana na dhana kwamba mimea na vitu visivyo hai havina akili/hisia tulizo nazo. Hii bila shaka ni kweli lakini haiondoi uwezekano wa aina fulani ya utambuzi au ufahamu.
Nguvu kama vile mvuto wa “gravity” na sumaku-umeme hutenda na hutokea kati ya vitu, ambayo ni aina ya mawasiliano, hata kwenye umbali mkubwa. Hivi karibuni imegunduliwa kuwa miti inaweza kuwasiliana kwa kutumia mizizi na mtandao wa fangasi (fungi) walioko chini na ndani ya ardhi. Nadharia za hivi punde kuhusu atomi zinapendekeza kwamba zinaonekana pia kuwa na uwezo wa kuathiriana kwa kutumia njia ambazo bado hatujazielewa.
Wacha tuchukue hatua ya ujasiri na kupendekeza kwamba ikiwa chombo au kitu kinaweza kuathiriwa na kuguswa na msukumo wa nje basi kwa njia fulani kina fahamu.
Kwa mtazamo wa mafundisho ya kidini, Fahamu inaweza kueleweka kama njia ambayo Mungu anamjua Mungu. Kama binadamu tumepewa vifaa vizuri vya kutuwezesha kufahamu mazingira yetu ya karibu. Pia tuna uwezo wa kutafakari uhusiano uliopo kati ya kile tunachojiona kuwa ni sisi na mahali petu katika ulimwengu.
Tunapoanza Kutahajudi kwenye Mwanga na Sauti haraka tunatambua kwamba sisi ni zaidi ya vile tulivyokuwa tunafikiria. Safari ya Kiroho ni upanuzi wa Ufahamu ambao hatimaye inaongoza kwenye Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment.
Cha Ajabu, hakuna Ufahamu wa chochote kwenye Hali ya Ukombozi wa Ufahamu kwani hilo lingehitaji utengano!
12 Novemba 2021
Unauliza kuhusu Ufahamu.
Hili ni swali zuri sana. Yote yanahusiana na jinsi wanadamu wanavyohusiana na mazingira yao. Watu wengine wangeishi maisha yao kisilika na wanachofahamu ni seti ya mifumo wanayoitumia kuishi maisha yao. Unaweza kusema kwamba wanatawaliwa na seti ya mifumo hiyo na wangehisi kutofurahi na wasiwasi ikiwa watapingwa, wako “salama” ndani ya mipaka yao.
Kuna wengine, hata hivyo, ambao wana changamoto na kupinga mipaka ambayo jamii inawawekea na “kutoka” kwenye ukungu. Wana mawazo yao wenyewe kuhusu wanavyopaswa kuishi maisha yao na hivyo ufahamu wao unapanuka ipasavyo. Hii ni picha na mfano rahisi sana wa suala gumu sana. Kila mtu ni kiumbe binafsi ambaye huongeza ufahamu wake kwa njia tofauti, lakini inasaidia kuwaelewa binadamu kama wale wanaokubali hali ilivyo na wale ambao hawakubali.
Sasa tumefikia sehemu ya kuvutia…….
Katika zoezi la Kutahajudi inawezekana Kuwa na Fahamu bila kuwa na ufahamu wa uchochezi wowote toka nje. Hii hutokea wakati mtu anakuwa mmoja na kile anachofanyia tahajudi au “meditation”.
Ni wazo na kitu kigumu kwa mtu yeyote kuelewa ikiwa hajawahi kuwa na uzoefu huu. Inawezekanaje kuwa na ufahamu kabisa, na bado hakuna kitu cha kufahamu!
Lakini watu zaidi na zaidi wanapitia uzoefu huu nje ya Tatahajudi. Kila inapotokea Ufahamu wao hupanuka Kiroho na Maarifa yao ya Ulimwengu wa Juu huongezeka. Ni kama kupasua pazia ambalo hawajui lipo.
Hii inaweza kutokea kwa mtu yeyote wakati wowote, hata kwa watu ambao kwa kawaida hawana nia ya kuondolewa katika eneo lao la faraja. Inatia moyo sana na inaweza kusababisha kubadilisha maisha – kimiujiza watu wanaweza kuona Ulimwengu kwa mtazamo tofauti kabisa na wanataka kuchunguza Maarifa haya mapya.
Maisha Duniani yana uwezekano usio na kikomo. Ufahamu wa mtu unaweza kupanuka Kiroho hadi Upanuzi wa Mwisho, ambapo inawezekana Kutambua kwamba kuna Ufahamu mmoja tu – Yeye!
Ukombozi hutokea wakati Ufahamu Unapojitambua Wenyewe.