Maana ya Ukombozi Wa Ufahamu au “Enlightenment” ni Hali ya Kuwa.
Anapopata Ukombozi Wa Ufahamu au “Enlightenment” Mtafutaji huvuka Ngazi zote za Ufahamu na kuunganishwa na Umoja unaoenea katika Uumbaji wote. Katika Umoja:
- Hakuna Mwanga.
- Hakuna Sauti.
- Hakuna wakati.
- Hakuna kushoto, kulia, juu, chini, mbele au nyuma.
- Hakuna maumbo, sura au rangi.
- Hakuna mipaka.
Muhimu zaidi hakuna wewe! Ukombozi Wa Ufahamu au “Enlightenment” haishuhudiwa kamwe kwani hiyo ingemaanisha utengano na uwili. Kwa mlinganisho ni tone la mvua kuunganika na bahari.
“Enlightenment” au Ukombozi Wa Ufahamu unafafanuliwa vyema zaidi kuwa Hali ya Upendo Usio na Masharti.