Nini Kinafuatia Baadaye!

 

Ni jambo la kawaida kuuliza maswali kama vile: Nitapata faida gani kwa Kutahajudi, Nitaona nini, Nitasikia nini.

Hatutaki kuwapa dhana nyingi sana na mawazo kabla ya Kuanzishiwa. Tunataka wewe ugundue mambo mwenyewe. Pia tunatambua kuwa kila Mtahajudi ni tofauti na yeye binafsi atagundua kile alicho na haja ya kugundua. Ni kama kozi ambayo imetengenezwa mahsusi kwa ajili ya mwanafunzi fulani.

Hata hivyo, tunahisi pia kwamba maelezo kidogo yatakuwa ya manufaa na msukumo wakati huu. Kwa hiyo tutaonyesha, kwa ujumla, nini kinafuatia baadaye!

Kwa kupitia njia ya ufunuo wa Mwanga wa Kiroho utakuwa na ufahamu wa jamii ya Maumbo na Rangi ambazo ni kielelezo ‟reflection” ya ufahamu wako wa maumbo katika Dunia.

Kwa kupitia njia ya ufunuo wa Sauti ya Kiroho utakuwa na Ufahamu wa sauti nyingi sana za mizunguko na mitikisiko mblimbali ambayo tena ni sawa na zile zinazopatikana katika ulimwengu wa kidunia.

Ulimwengu wa kimwili ni makazi ya aina nyingi ya viumbe mbalimbali vyenye akili na kwenye ngazi za juu za Ufahamu kuna idadi kubwa ya Viumbe wa Kiroho. Kwa hiyo, kuna uwezekano wakati fulani utakuwa na mawasiliano na Viumbe hawa na kupokea Maarifa na Ujuzi mkubwa.

Safari tunayoongelea ni safari ya Ufahamu ambayo Asili ya Kile ambacho ni Wewe Kweli kinagunduliwa na uhusiano wake na ngazi za Maumbile. Maarifa hayatolewi kwa njia ya ufahamu wa chini (ambao ni matokeo ya akili) lakini kwa ‟ Ufunuo” moja kwa moja.

Utagundua kwamba mtazamo wako unahama na kukuwezesha kufahamu “Picha kwa Ujumla”. Hii kwa itakusaidia kuelewa maana ya, na kuunganisha Utambuzi (‟realizations”) wako.

Hatimaye wakati Njia hii ikifunuliwa itakupa lengo la Mwisho ambalo litajitokeza kama Amani, Furaha na bila shaka LOVE.