Walimu ambao ni ‟Enlightened”

 

Tunafuraha kutangaza kwamba idadi ya Walimu ambao wana Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho ‟Enlightened” inakaribia mia mbili.

Uongozi wa Kiroho walitabiri kuwa Kundi letu linapaswa kufikia 75,000 katika kipindi cha miaka michache ijayo. Ili kuwachukua watu hawa pamoja kwenye Njia ya Kiroho kwa muda mfupi hivi Wao wametupatia idadi kubwa ya Walimu na Watahajudi ambao wanaweza kupitisha Cheche za Mungu kwa wengine.

Ukuaji zaidi wa sasa imekuwa Amerika ya Kati na Kusini na imevutia watu kutoka asili mbalimbali na kutoka makundi yote ya umri. Baadhi walikuwa na uzoefu kidogo wa kutahajudi au hakuwa na uzoefu kabla ya Kuanzishwa kwao. Hata hivyo walivutwa, wakati mwingine kimiujiza, kwenye Kundi na kuungana kiasili na Nguvu kana kwamba walishawahi kutembea Njia hii kabla!

Wengi wa watu wapya waliopata Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho wana mawasiliano moja kwa moja na Uongozi wa Kiroho na wanaongozwa kueneza ‟WimbiMwanga” (Lightwave) mpya katika maeneo wanamoishi. Wengine wako kwenye maandalizi ya kusafiri ili Nguvu zifike Nchi jirani.

Ushirikiano katika kiwango kikubwa kiasi hicho hakiwezi kushindwa kutengeneza Miujiza!