Ushuhuda (M.T.)

 

‟Initiation” yangu ilikuwa mnamo tarehe 10 Septemba, 2016. Kabla ya kutahajudi kwenye Mwanga na Sauti nilikuwa na muda wa kutosha bila kutahajudi hivyo mwanzoni ilikuwa kidogo vigumu kwangu kuwa makini na kutulia. Lakini wakati huo ambapo mimi nilikuwa naenda kutambulishwa na kuanzishwa kwenye Mwanga, hatimaye niliona kwamba naweza kutulia kwa makini na ku‟concentrate” kwa msaada wa kurudia Mantra yangu.
 

Wakati walimu wangu wa Kiroho waliponipatia Mwanga kila kitu kilibadilika, Nilihisi kitu, sikuweza kufikiri mtu anaweza milele kujisikia hivho. Nikawa Mwanga, nilikuwa si Melanie tena, mimi nilikuwa “Mwanga wa Jua”, nilijihisi kama kitani kidogo kinachounganisha Dunia na Jua. Kila kitu ndani yangu kilikuwa Cheupe, mawazo yangu yote, hisia zangu, ngozi, kila kitu. Wakati huo nilitambua kwamba nilikuwa mwili wa binadamu duniani lakini akili yangu, nafsi, na Roho zilikuwa Mwanga. Nilikuwa sehemu ya vitu viwili vya ajabu, Dunia na Jua kwa wakati mmoja, vilivyounganishwa pamoja. Hivyo ndivyo nilivyojua mimi ni Mwanga na sisi wote pia!
 

Baada ya kuuhisi Mwanga mimi nilihitimisha kwamba inawezekana kuwa hakuna hisia yoyote ya ajabu zaidi kama ile. Lakini ilikuwepo wakati Sauti ilipokuja…..
 

Wakati nilipopokea Sauti nilisikia na nilihisi ukamilifu mkubwa ambao sijawahi kusikia au kuhisi milele. Kwa wakati ule hakuna kitu ambacho kilikuwa cheusi au cheupe, mzuri au mbaya, kizuri au kibaya, furaha au huzuni, hai au kufa. Kila kitu na kila mtu alikuwa tu, bila hukumu na fikra.
 

Kwa mfano: wewe ni mmea mdogo ambao daima umeshikamana na dunia kwa kutumia mizizi yako na umeshikamana na hewa na kwa kutumia majani, lakini wakati wa kupokea Sauti wewe ni mmea bila hewa au ardhi. Wewe ni mmea lakini baadaye unatambua kuwa mmea hauwezi kuishi bila hewa au ardhi, hivyo mimi nilipata hitimisho kwamba mmea si kitu bila mambo haya mawili lakini ni kila kitu ikiwa na hewa na ardhi. Hivyo sisi ni Kila kitu ambacho kweli si Chochote!
 

Mwanga ulikuwa wa ajabu na akili-mbiu lakini Sauti kweli ilikuwa ya ajabu sana. Najisikia furaha ya kweli na kwamba nilikuwepo mahali pazuri na bora kwa muda muafaka ili niweze kupokea ‟Initiation”. Pia nawashukuru walimu wangu wa Kiroho ambao wamenisaidia kujua mimi ni nani. Mimi kwa kweli natumaini kuwa kila mtu ataweza kutahajudi kwenye Mwanga na Sauti katika maisha yao.
 

Upendo (M.T.)