Tunapoangalia ukubwa wa ulimwengu ni vigumu kudhani kwamba binadamu anawakilisha kilele cha maisha ya Viumbe wenye akili. Kama pia tunafikiria uwezekano wa kuwepo kwa “Dimensions” zingine basi hatuna budi kufikiria kwa uzito uwezekano wa kuwepo kwa Viumbe ambao wanatuzidi sisi wote kitaalam na kiakili.
Viumbe wanaoishi kwenye ulimwengu wa kimwili (physical universe) na kufungwa na sheria zake watapambana sana kuwasiliana na wenzao kutokana na umbali mkubwa unaohusika. Inaonekana kuna upeo wa kasi na mwendo ambao unajulikana kama kasi ya Mwanga. Aina zote za mawasiliano kama vile mawimbi ya redio, lasers na microwaves huzingatia sharti au sheria hii. Kwa kasi hii ya mwanga, ishara (signals) zitachukua miaka 4 kufika kwenye nyota iliyo karibu sana nasi na miaka milioni 2.5 kuwasili kwenye Galaxy iliyo karibu yetu.
Takwimu hizi zinaonyesha ugumu wa kusafiri zaidi ya mipaka ya mfumo wetu wa jua yaani solar system. Kama tusipoweza kupata njia nyingine ya mawasiliano ambayo inazidi mipaka ya mwanga, basi tumetengwa kwa ufanisi haswa kutoka kwa Viumbe wote ambao wanaweza kuwepo katika vilindi vya nafasi (space).
Kuna matumaini yanajitokeza kwa sababu ya matukio na ugunduzi wa jambo lililoitwa ‟entanglement”. Hii inapendekeza kwamba baadhi ya chembe ambazo ni ndogo kuliko atom ‟subatomic” kama vile elektroni zinaweza kuwasiliana, papo hapo! Pia kumekuwa na dhana kuwa ubongo inawezekana unafanya kazi kwa njia hii.
Hii inasababisha uwezekano wa kusafiri kupitia na ndani ya ‟Dimensions” nyingine. Wanasayansi wengi wanaamini hizi ni njia rahisi tu na mbinu ‟fudge” ya hisabati lakini kuna kundi kubwa la watu ambao wanadhani hizi “ulimwengu nyingine” zipo kweli kama hali halisi kabisa.
Watu ambao wanatahajudi kwenye Mwanga na Sauti hutambua kwamba Nguvu au Nishati hizi asili yake sio ya kimwili (physical). Ni kana kwamba huonekana kwa macho mengine na kusika kwa masikio mengine. Ni kawaida kuwa na ufahamu wa sauti ya kimwili (physical) na wakati huo huo kuwa na ufahamu wa Sauti ya Kiroho. Hii inaweza pia kutokea kwa mwanga wa kimwili na Mwanga wa Kiroho. Labda inaeleweka bora kama upatikanaji wa hisia nyingine mbili zaidi.
Pia inakuwa wazi sana kwamba hatuwezi kudhibiti Nguvu za Kiroho; mara tunapojaribu kuziweka kwenye akili ‟intellectualize” hutoweka. Wakati tukiwa na tamaa na mategemeo, Zinarudi hazionekani. Huonekana kusubiri hadi tujitokeze tukiwa wazi, wanyenyekevu na heshima. Tunapokuwa na mtazamo sahihi basi tunachukuliwa kwenye Safari. Safari hii hatimaye husababisha Enlightenment ya Kiroho, Maarifa Kamili ya kile kinachoweza kuelezeka bora kama Umoja Kamili wa Jumla.
Wakiwa Njiani na baada ya Enlightenment Watahajudi wengi huripoti kuhusu Viumbe Wa Mwanga. Viumbe hawa wana Upendo usioweza kuelezeka na wakati mwingine hutoa Mafundisho na Maarifa. Hii inaweza kuwa msaada wa matatizo ya kibinafsi au hata maarifa ambayo yameundwa ili kusaidia Dunia na wakazi wake. Hivi ndivyo Njia hii ilivyoanza mnamo mwaka 2015!
Kama binadamu, sisi wote tuna uwezo wa kupenda na kuonyesha huruma kwa wengine. Baadhi wanaweza kukataa na kusema hii ni kwa sababu tunataka kulinda maslahi yetu, lakini hii haielezei kuwajali wengine ‟Atruism” na wale ambao hutoa bila kujulikana. Kama tunaweza kuonyesha sifa hizo nzuri, ina maana kwamba hata Viumbe kutoka kwenye Ngazi za Juu pia wanataka kufanya hivyo.
Wanavyoshuhudia hatma ya dunia na wakazi wake Wao kwa kawaida wanataka kusaidia. Njia moja ya kusaidia inakuwa kutuonyesha sisi Ngazi Hizi za Juu wanapoishi, kuwa kweli zipo na hakuna njia bora zaidi ya kufanya hivyo, kuliko kutupa uwezo wa kutembelea Ngazi hizi. Hii bila shaka ni Njia ya Kiroho ambayo wengi walitembea kwa miaka mingi iliyopita. Pia ni msingi wa karibu Dini zote.
Leo, inaonekana kwamba watu wa kawaida wanakuwa na ufahamu wa Nguvu/Viumbe hawa kana kwamba wanaamshwa. Kwa wengi hii ni faraja sana na inasaidia kuyapa maisha yao maana ya Kiroho. Kwa wengine wanaona kama mwaliko wa ajabu kujiunga na kutafuta Njia ya Kiroho na kugundua Maajabu Yasiyo semeka.
Wasiliana nasi kama unataka kusaidiwa kufikia Mwanga na Sauti au kama tayari una ufahamu wa Nguvu hizi na ungependa kujifunza jinsi ya Kutahajudi kwenye Nguvu hizi.