Siku 3 – Tarehe 1-3 Januari 2018 Ni asubuhi saa nne na dakika 57 (10:57 am) tu, siku ya tatu ya siku tatu za kutahajudi. Leo asubuhi, kwa staili ya Hollywood ya ajabu, nyota za uumbaji zilinichukua mimi kwenye safari ya ajabu kwenye mipaka yote ya kuwa na kwingineko.
Niliomba kuwa Enlightened siku ya kwanza. Lakini jana ilikuwa siku ngumu, sikuweza kuwa makini, akili yangu ilikuwa kwenye takataka ya mawazo – kutoka kwenye kin’gan’ganizi cha mawazo yangu ya sasa hadi mtiririko wa mawazo nisiyo na ufahamu nayo pamoja na hisia … mawazo yasiyo tabirika, uhusiano ila mvurugiko wa mawazo. Si ajabu kuwa dunia iko katika hali kama hiyo kama akili ya kila mtu ni kama hii, niliwaza.
“Haitatokea kwangu. Siwezi kutahajudi. Watu wengine wana tahajudi nzuri na wazi. Lakini akili yangu haifanyi kazi hivyo. Basi! Ni wazi hiyo ndivyo ilivyotakiwa kuwa … ..sio kwangu kwenye maisha yangu haya. Lakini ninawaangusha watu ambao wamejitolea na kutoa huduma na upendo wao kunisaidia mimi.” Na pia nilikuwa najiangusha mimi mwenyewe.
Hivyo mimi niliacha kutahajudi mapema jioni na kwenda kulala, nikiwa nimekata tamaa.
Asubuhi hii, niliamka na viumbe bora wa uumbaji, wakiwa tayari kunisaidia – wakiwa kwenye johari la mwanga unaong’aa. Kiumbe Mmoja alikuwa upande wa kushoto kwangu na moja ambaye haonekani (lakini nilimhisi) alikuwa upande wa kulia. Kulikuwa na umati wa wengine. Niliamka na kutahajudi nikifuata uongozi wao, bila kuhoji, kwani nilijua nilikuwa katikati ya kitu maalum.
Mara baada ya kufumba macho yangu nilikuwa na hisia ya kupanda “juu” kwa haraka. Mara moja kila kitu “kililipuka”. Na katika wakati huo kila kitu kilibadilika … ufahamu kuhusu maisha, na kisha amani.
Kulikuwa na ufa wa mwanga mkali. Uwezekano wote ulikuwa hapa. Nilichezea na kuusambaza mwanga, unaowasha “helixes” mbili za DNA yangu. “Nilituma” mwanga kwa watu walio karibu nami na wale ambao nilijua wanahitaji msaada. Na kisha nilitahajudi na kujiachia nakujisalimisha kwenye amani.
Hatimaye nilichukua mapumziko ya kutahajudi na niliporejea …
… ishara nyingine ya kuendelea kupanda kwenye ufa wa mwanga. Nilijiuliza nini kitatokea. Ningependa kufa kwenye ule Mwanga – kuyeyuka na kutoweka. Nikasita kwa muda… .. hofu …… .. kisha kwenye mwanga. Nilijikunja kama mpira ili kutosha kwenye ufa, na kuwa kijusi na kuyeyuka kwenye mwanga. Kisha mimi nilikuwa cheche ndogo tu ya mwanga. Kisha nia tu … .. Kiini (Essence). Na kisha …
“Mimi ndiyo Mwanga.”
Kisha “nyuma” zaidi.
Kabla ya Mwanga.
Na kisha …
“Mimi
Sio Kitu”
Hakuna nafasi, hakuna muda, hakuna kilichopatikana, hakuna kilichopotea, hakuna hamu, hakuna joto, hakuna baridi, hakuna rangi, hakuna utupu, hakuna karibu, hakuna mbali, hakuna juu, hakuna chini, hakuna weusi, hakuna weupe.
Hakuna ukosefu.
Utulivu. Kamili.
A m a n i K a m i l i.
……
Mtu mzee asiyeweza, ambaye si wa kawaida, na mwenye dosari, kasoro, mtahajudi mbaya mimi. Utando mgumu wa fumbo tukufu la maisha umenyoshwa na kuvunjwa. Na katika wakati huo ……. hatima yangu kutimia.
…..
Hitimiso
Kila kitu kinatokea kama kilivyo. Niliomba Enlightenment na najua “Masters” na Viumbe wa juu wa uumabaji waliweka kila kitu katika nafasi yake ili kufanya itokee kwangu. Ingawa kimawazo sio kitu ambacho mtu ungetarajia kabisa. Ingawaje inasikika kama ukichaa, ilichukua umati wa Viumbe na mwanga unaong’aa kuweza kunifikisha pale.
Lakini ilifanya kazi – kuniweka makini, na kunisaidia kujisalimisha. Zawadi ya Neema tupu.
Tangu siku ile ya ajabu, tahajudi imekuwa ya ajabu – ya nguvu, kuleta mabadiliko na mkazo uliojazwa na Upendo. Naamini kuwa kile ambacho binadamu anahitaji kujua kiko pale tayari kugunduliwa …. kuhusu kila mada iwezekanayo kufikirika na ambayo bado kufikirika. Kwa “kuleta chini” maarifa ya kubadili dunia hii. Kuishi kwa huruma, uzuri na heshima. Na kwa upendo … bila masharti. Na kadri watu zaidi wanavyofikia Enlightenment, ndivyo mabadiliko, upendo zaidi, na hekima ya juu zaidi.
Mwanzoni niliamini kwenye umri wa Enlightenment na kisha niliacha kuamini. Sikuweza kuona jinsi ambavyo binadamu wangeweza kufikia kiwango hiki.
Lakini sasa naweza!