Madhumuni ya Njia (Tahajudi)

 

Madhumuni ya awali ya Njia hii ya Kiroho ni kwa ajili ya Mtafutaji kupewa upatikanaji wa Ngazi za Juu za Ufahamu ambazo huonekana kama Mwanga na Sauti nzuri za Ndani. Kwa Kutahajudi kwenye Nguvu hizi mtu hujifunza kuhusu Siri za Ulimwengu na kuanza kutambua Asili yao ya Kweli. Hii ni zaidi ya nyanja za kimwili, kihisia na kiakili. Sio kitu ambacho kinafundishwa na kinahitaji imani … ni kitu kinashuhudiwa na ni Ujuzi na Maarifa Kamili.

Hatimaye, Njia hii inafikia upeo kwenye Enlightenment. Mtahajudi atavuka ngazi zote za Mwanga na Sauti na kuunganishwa na ‟Infinite”. Hii mara nyingine inajulikana kama Ufahamu wa Mungu. Baada ya kufikia Hali hii Mtafutaji atatambua Siri ya Mwisho…..Ulimwengu umejazwa na Nishati moja tu ambayo ni Upendo. Kutoka kwenye Upendo huu kinajitokeza kila kitu kwenye Maumbile yote ambayo hutiririka kupitia na kwa njia ya Ngazi Kubwa Mbali Mbali za Kiroho na hatimaye hutengeneza mazingira ya kimwili ambayo tunayoyaelewa.

Baada ya kufikia Hali hii (Enlightenment), kitu halisi ambacho mtu anaweza kufanya, ni kutoa. Kutoa kunaweza kuwa kwa njia nyingi. Kunaweza kuonyeshwa kwa kutumia “Kanuni ya Kulipia Baadaye” au “Pay it Forward Principle” kwa kuwasaidia wengine kugundua Asili yao ya Kiroho. Kuna watu wengi wanaosumbuliwa wakati huu wa sasa ambao wangefaidika na Huruma na wema tu. Pia, Dunia inaumwa sana kutokana na karne nyingi za matumizi mabaya; kuna miradi mingi ambayo inaweza kusaidia kurejesha usawa maridadi wa Asili.

Dunia ni mahali pagumu na maisha hapa si rahisi. Tunaendeshwa na kupambana kila siku ili kuhakikishia maisha yetu. Mara nyingi tunakuwa na matatizo ya afya zetu. Tunaweza kupambana kwenye uhusiano, ajira na masuala ya fedha. Tungekuwa na nguvu za kichawi (magical powers) basi kila kitu kingeweza kuwa sawa.

Hata hivyo, lengo la maisha ya kimwili ni kujifunza masomo na baadhi yao ni magumu na yanahitaji kiasi fulani cha mateso. Njia ya Kiroho haikufanyi ukwepe matatizo na sio ufumbuzi wa matatizo yetu yote ya Duniani. Inachotoa ni mtazamo mpya kabisa ambao tunaweza kuona njia za kupunguza na / au kutatua baadhi ya matatizo yetu.

Mtu akikwambia kuhusu tatizo lake linalomsumbua mara nyingi unaweza kuona ufumbuzi rahisi kwa sababu mtazamo wako ni ‟neutral”, hauna upande au nia yoyote. Hali kadhalika inawezekana, kwa njia ya Kutahajudi, kuwa na mtazamo sahihi wa matatizo yako mwenyewe, na hivyo kufanya iwe rahisi kuweza kukabiliana nayo na kufikia ufumbuzi na mafanikio.

Hivyo kuhitimisha, Njia ya Kiroho itakufunulia na itakuonyesha Asili yako ya Kweli na kufungua Siri nyingi za Ulimwengu. Wakati huo huo, bado una jukumu la kuongoza maisha yako ya kimwili na kuvumilia masomo yake mengi. Hata hivyo, Ufahamu wako unavyozidi kupanuka itakuwa rahisi zaidi kukabiliana na changamoto ambazo zitakuja kwako.

Kwanza ni huduma ya binafsi na kisha huduma kwa wengine. Unavyojifunza kutoa zaidi, ndivyo ambavyo lengo lako linakuwa mbali na ubinafsi wako na ndivyo zaidi unaweza kutimiza lengo la maisha yako.


“Kutoa tu ndio kunakufanya ulivyo.”