Mifano ya Kiroho

 

Tunapojaribu kufikiria na kuelewa Ulimwengu wa Kiroho kwa ujumla tunafanya hivyo kwa njia ya msaada wa baadhi ya mifano. Kwa kawaida hiki ni kitu ambacho tumefundishwa au kusoma katika kitabu.

Baadhi ya watu wanaweza kuchagua kugawanya Ulimwengu wa Kiroho kwenye mikoa, wengine huwa na taswira ya ngazi kama tabaka ya mwamba wakati wengine wanaweza kujaribu kuwaza kwamba kila kitu kinaingiliana.

Linapokuja suala la Viumbe wa Kiroho, watu watawaona Viumbe Hawa kwa njia tofauti, kwa mfano: katika umbo la binadamu, kama maumbo ya Etha (”Ethereal”), kama matone makubwa ya Mwanga au kama uwepo wa nguvu.
Hivyo tunaweza kuuliza, ni ipi hapo juu ni Sahihi? Ipi ambayo ni mfano bora? Je, Viumbe wa Kiroho kweli wanafanana vipi?

Jibu: Hakuna hata moja hapo juu!

Ni majaribio yetu ya kuelewa kitu ambacho hatuna uwezekano wa kukielewa. Daima Uongozi wa Kiroho wanatukumbusha hili.

Huwezi kufikiria ni jinsi gani ilivyo kuwa hapa. Huwezi kufikiria jinsi gani na idadi ya viumbe walioko katika Mbingu za Kiroho.

Hilo likiwa akilini, je, ni kosa kutengeneza hii mifano? La hasha! Tunahitaji kitu kinachoonekana ili tuweke ”realizations” zetu juu yake na kutupa maana ya Njia yetu na maisha yetu ya duniani kuhusiana na jambo hilo. Pia inaturuhusu sisi kuwa na njia ya kuweza kuzungumza na watahajudi na watu wengine ambao tungependa kuwatabulisha na kuwaanzisha kwenye Njia hii.

Kumekuwa na majadiliano mengi hivi karibuni yanahohusu ”negativity” na mifano mbalimbali kujaribu kuelezea. Tunajua ipo na tunahisi tunahitaji kufafanua inatoka wapi, asili yake na jinsi ya kukabiliana nayo.

Wakati tunauliza maelezo kutoka Uongozi wa Kiroho, Wao hutoa maelezo kwa lugha yetu, kwa njia ambayo tunaweza kuwelewa na kwa kawaida ikiwa katika mfano ambayo tayari tumejijengea. Kama sisi tukiomba habari, Wao kwa ujumla kutupatia taarifa. Hata hivyo, sisi ni binadamu binafsi na tuna mipaka na upendeleo;Imesemekana kuwa tunahitaji kuwa ”neutral” wakati sisi kushusha au tunatuma ”channel”. Hii karibu haiwezekani, sisi ni sisi, pamoja na chuki zetu zote na ”polarizations”. Majibu tunayopokea yataonyesha hilo.

Hebu tusifanye makosa ya dini ya kumtengeneza Mungu kwa mfano wa mwanadamu. Hebu kujifunza kutoka kwenye sayansi iliyochukua mfano wa Dunia inayozunguka Jua sio kwa sababu ilichukuliwa kuwa kweli (wakati huo) lakini kwa sababu ilifanya kupiga mahesabu ”navigation” kuwa rahisi.

Kwa hivyo ni jukumu letu, kama watu binafsi, kutumia mifano na maelezo ambayo tunafarijika nayo. Sio lazima kwa sababu ni ya kweli, lakini kwa kuwa tunajisikia na kuona ni sawa kwetu. Hakuna sababu ya kutumia kiasi kikubwa cha muda kulalamikiana kuhusu mitazamo tofauti na falsafa. Tunaishi katika Dunia ya mitikisiko na majanga, tunahitaji kuwa makini kwenye njia zetu za binafsi na kusaidia wengine kufanya hivyo. Muda unakwenda!


Ukweli pekee wa Kweli uko ndani Yetu.