Unyenyekevu ndio Ufunguo

 

Dini na falsafa nyingi zinapendekeza kwamba Asili ya Mungu ni Umoja. Watu wengi duniani huamini kwamba hii pengine ni sawa na kweli.

Kwenye Njia hii kamwe hatuhimiza imani kwa sababu nia ya Njia ni kujigundua mwenyewe au ugunduzi wa kile ambacho ni wewe. Sio muhimu kile ambacho watu wengine wanajua, kilicho muhimu haswa ni nini unajua. Sio kama zoezi la akili lakini Ufunuo wa Elimu ya Kiroho Kamili – na Ufunuo binafsi.

Kile utakachogundua ni sawa kama Watafutaji wote waliofikia Enlightenment… Umoja Kamili bila Mipaka … Nguvu ambayo inaweza kuelezewa vizuri kama Upendo Kamili ulioenea na kusambaa kwenye Maumbile yote.

Kweli ni rahisi kiasi hicho. Ndio maana sisi hatujaribu kuwasilisha mafundisho yoyote magumu au kuhimiza mila tata au mazoea tata. Sisi hufunua na kufichua tu Nguvu ya Mwanga na Sauti ili Mtafutaji aweze kuongozwa kwenye Chanzo.

Watu wengi wanapenda kujadili masuala ya Kiroho yaliyofichika; idadi kubwa ya vitabu vimeandikwa juu ya suala hili. Hata hivyo Hali na Asili ya Maisha ya Kiroho ni zaidi ya maneno au mawazo yote. Huwezi kufikiria njia yako kwenda kwa Mungu.

Kwa hiyo, jaribu kudumisha unyenyekevu wakati wote. Angalia maisha yako na kutafuta njia ya kufikia maelewano na kupunguza utata. Wakati unapotahajudi kubali badala kuuliza, yeyuka badala kuchambua na Upende badala ya kufikiri.


Ni Ufunguo wa Unyenyekevu tu ambao utafungua mlango wa Umoja.