Njia ya Tahajudi ya Mwanga na Sauti ni nini?
Mwanga na Sauti ni Nguvu zinazojumuisha ngazi za juu za Ulimwengu wa Kiroho wa Kweli. Ngazi hizi za maumbile ni zaidi ya ulimwengu wa kimwili ambao ni pamoja na mwili, hisia na cha muhimu, zaidi ya mawazo yote. Hizi ngazi za Maumbile ndio Chanzo cha kila kitu ambacho sisi kwa kawaida tunatambua na kuna Viumbe wenye Akili na Ufahamu ambao tunawaita Uongozi wa Kiroho.
Njia ya Tahajudi ni Safari ya ugunduzi wa kibinafsi ambayo inamchukua Mtafuta kupitia Ngazi mbalimbali za maumbile ya Kiroho na hatimaye kuelekea kwenye Hali kamili ya ‟Enlightenment”.
Uongozi wa Kiroho ni nani?
Mabwana (Masters) wote, Gurus na Walimu wa Kiroho huongozwa na Viumbe wenye Ufahamu na akili ambao wapo kwenye Ngazi hizi za Juu za Maumbile. Wao ni Chanzo cha Hekima zote na Maarifa ambayo yamewahi ‟kushuka” kwenye akili za Wanadamu kwa karne zote. Ni kupitia kwao ambapo kumewezesha Ufunuo wote wa Kiroho kufanyika. Hii hutokea, wakati mwingine bila kutarajia, au kwa kutumia mbinu maalum au kupata ‟Initiation” au Kuanzishwa.
‟Initiation” au Kuanzishwa ni nini?
Utumaji na Uhamisho wa Nguvu za Kiroho kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine tunauita ‟Initiation” au Kuanzishwa. Walimu wetu ambao wamekuwa ‟Enlightened” wana uhusiano na Uongozi wa Kiroho unaowawezesha kuhamisha Mwanga na Nguvu za Sauti kwa wale wanaotafuta Kweli. Chanzo cha Nguvu hizi kiko katika Ngazi za Juu za Kiroho; Waalimu wetu wanakuwa kama viungo tu. Hakuna kikomo cha idadi ya watu wanaoweza Kuanzishwa isipokuwa vikwazo vya nafasi na wakati.
‟Enlightenment” ni nini?
‟Enlightenment” tunayozungumzia ni Hali Kamili ya Mwisho ya Ufahamu. Ni zaidi ya ulimwengu wa kimwili, hisia zote na muhimu zaidi, kuliko mawazo yote. ‟Enlightenment” ni zaidi hata ya Mwanga na Sauti yenyewe na ni Umoja Kamili. Haina umbo, sura, haina mipaka na haina wakati. Ni Chanzo cha Kila kitu ….Upendo Kamili Kabisa.
Je, mnae Kiongozi?
Hapana, Uongozi wa Kiroho uliwasiliana na idadi ndogo ya Watahajudi Waliokuwa ‟Enlightenment” na mnamo mwaka 2015 na wakawaomba kuanzisha Njia mpya ya Kiroho ambayo ingeleta Mwanga na Sauti kwa watu wote. Kila Mwalimu wetu hufanya kazi kwa kujitegemea. Hii inaepuka matatizo ya nguvu na ‟ego” ambayo huwa inayakabili makundi mengine mengi. Pia inampa kila Mwalimu uhuru wa kujieleza kwa kawaida kwani hawana haja ya kujiandikisha na kuwa wanachama wa mafundisho yoyote au ‟dogma” yoyote ile. Tunachowaomba tu ni kwamba wanakubaliana na kanuni zetu kuu za msingi.
Kanuni kuu za msingi ni nini?
- Hatuna Kiongozi, Waalimu wetu wa Kiroho wote hufanya kazi kwa uhuru.
- Tunajitolea na kuwaunga mkono watu wote ambao wanataka kugundua Ufahamu wa Hali za Kiroho kwa kutahajudi ‟Meditate” kwenye Mwanga na Sauti.
- Nguvu ya Tahajudi ya Mwanga na Sauti hutolewa kupitia Uongozi wa Viumbe wa Kiroho.
- Hakuna mahitaji ya maisha, ila mapendekezo tu ya kawaida.
- Hakuna ada yoyote, ama kwa ajili ya Mantra, Hali za Kiroho, au kwa mtu yeyote au shirika lolote. Tunatumia kanuni ya ‟Kulipa mbele”.
- Nguvu ya Tahajudi ya Mwanga na Sauti na ugunduzi wa Ufahamu wa Hali za Kiroho, inapatikana kwa watu wote katika nchi zote, bila kujali jinsia, hali, utamaduni, rangi au imani.
- Watu wanaochagua kutahajudi kwenye Nguvu za Mwanga na Sauti huweza kuendelea kwa kiwango chao wenyewe.
Kanuni ya Kulipa Mbele Ni Nini?
Kama ilivyoelezwa hapo juu, yote tunayoyatoa Kiroho, yanaonekana kama Zawadi na hivyo ni bure kabisa bila malipo yoyote. Tunatarajia, hata hivyo, kwamba wale wanaopokea Zawadi hii watataka wengine wawe na nafasi sawa kama wao wenyewe. Kwa namna hii wanaweza ‟Kulipa Mbele” kwa kusaidia watu kwenye jamii zao wanaotaka kutahajudi na kutafuta Ukweli.
Malengo ni nini?
Kuna malengo mawili, moja la mtu binafsi na la pili kwa Wote. Kwa mtu binafsi tunampa Mtahajudi fursa ya kuwa na Ufahamu wa Ngazi za Juu za Kiroho na uwezekano wa kufikia ‟Enlightenment”. Katika ngazi ya Wote tunawaomba Watahajudi ambao wamepewa uwezo wa kufikia kwenye Ngazi za Juu za Kiroho kutuma Upendo na Mwanga kwenye Sayari yetu kama sehemu ya mazoezi yao ya kutahajudi. Tumeambiwa na Uongozi wa Kiroho kwamba Sayari hii inaumwa sana na inahitaji usawazishaji wa nguvu. Aidha ni sehemu kubwa ya Ulimwengu kwa Ujumla ambayo inahitaji pia kuunganisha na maelewano.
Kwa nini Sasa?
Hivi sasa Sayari ya Dunia iko katika hali ya hatari inayoletwa na tamaa na ujinga wa wanadamu. Tunaambiwa kwamba kihistoria kumekuwa na majaribio mengi ya kurekebisha hali hii lakini mengi yameishia kushindwa kabisa. Kuna usawa maridadi kati ya Roho na ‟Matter” (Udongo) ambayo kwa wakati huu iko katika upande wa ‟Matter” (Udongo). Hii inahitaji kurekebishwa haraka iwezekanavyo kwa kuingiza Nguvu ya Kiroho kwa wingi kwenye Sayari bila kuchelewa. Ndiyo sababu Njia hii ipo na ndiyo sababu tuna uwezo wa kupitisha nguvu za Kiroho kwa urahisi; tunahitaji idadi kubwa ya Waanzishwaji ‟Initiates” na tunawahitaji sasa!