Vikundi Vingine – Mafundisho Mengine

 
Mara nyingi tunaulizwa maswali juu ya vikundi vingine na mafundisho mengine. Mara nyingi kuna mafundisho yetu fulani ambayo yanafanana na ya vikundi hivi, ikiwa ni pamoja na tofauti zilizo wazi. Inasisimua na kufurahisha kugundua kuwa Mafundisho yanawasilishwa kwa watu wengi walio wazi na nyeti, kote Ulimwenguni, kwa wakati huu.

Tatizo ni kwamba tofauti zinaweza kusababisha mkanganyiko na mijadala mikali. Wakati habari zinachapishwa na Walimu na/au Vikundi kwa, kawaida huwasilishwa kama Ukweli na Ukweli pekee.

Ni matumaini yetu kuwa, kwenye nakala hii, tutaweza kuwasilisha “Picha Kubwa” kuelezea tofauti hizi, na kukubaliana na maoni tofauti.

Hebu tufikirie watu wanaoishi katika jengo refu sana la gorofa, tuseme kama New York. Wale wanaoishi kwenye ghorofa ya chini wangekuwa wanajua vizuri msukosuko wa barabara. Wangeona mabadiliko ya maumbo na rangi nyingi kila wakati zikiambatana na sauti nyingi; ingewezekana kusoma ishara na kusikia mazungumzo ya kibinafsi.

Mtu anayeishi gorofa za juu atakuwa na mtazamo tofauti kabisa. Angeweza kuona mbali zaidi na kujua mtandao wa barabara. Mwendo na harakati za magari na watu hautakuwa mkubwa sana na sauti zinaweza kujumuika nyuma ya sauti zingine, ikawa mara chache akasikia honi za magari.

Ikiwa sasa tutahamia kwenye gorofa ya juu kabisa, mtazamaji ataweza kuona jiji kuhusiana na Bahari ya Atlantiki, mto Hudson na vilima vya mbali. Akiangalia chini, kungekuwa na mwendo dhahiri mdogo sana na sauti pia zingekuwa kwa mbali na kidogo sana. Hata hivyo, ndege (aeroplanes) na ndege hai warukao juu, pamoja na mawingu na vivuli vyao sasa vingetuvutia.

Hiyo hapo juu ni mliganisho, mfano au (analogy) ya Viumbe wanaokaa katika Maeneo au Ngazi za Kiroho. Tunaambiwa kwamba kila Ngazi au (Dimension) ya Uumbaji imejaa Viumbe wengi. Kila Kiumbe akiwa na mamlaka yake mwenyewe na misheni au lengo yake, Kikundi ambacho huwasiliana na watu kwenye Sayari hii kutoa Maarifa na Elimu ya Kiroho. Kikundi cha Meditation ambacho tunawakilisha kimehamasishwa na Kundi hili; tunaowaita kwa jina la Uongozi wa Kiroho. Wana Ujumbe na lengo maalum, la kuunganisha watu wengi iwezekanavyo na Mwanga na Sauti ya Kiroho na kukuza Uamsho wa hiari bila kutegemea.

Tunachohitaji pia kuelewa ni kwamba Viumbe Wengine Wana ajenda zao. Hii inaweza kuhusisha, kwa mfano, kufanya kazi na Nguvu za Kiroho ili kusaidia kuponya Sayari yetu au kuwasiliana na viumbe vya kimwili katika mifumo mingine ya Nyota au Galaksi. Kila moja ya Viumbe hawa wa Ngazi za juu ana mtazamo wao na Wanatoa maoni Yao ipasavyo. Kwa sababu watu watakuwa wakipokea Ujumbe kutoka kwa Vyanzo tofauti, hii bila shaka itasababisha kuchanganyikiwa kwa kiasi fulani. Kamwe sio swala la nani yuko sahihi na nani amekosea; ni kiasi tu cha kutambua kwamba kutakuwa na mitazamo tofauti, kama mfano wa gorofa ndefu unaonyesha wazi.

Ikiwa tunatafuta Hekima basi tunapaswa kuwa wazi kwa Mafundisho yote ambayo tunapata. Wakati huo huo tunapaswa kuzingatia habari kwa uangalifu na kuona ikiwa habari hiyo inaweza kuingizwa kimaarifa katika uelewa wetu wa sasa. Tunapaswa pia kujua kwamba ni tabia ya binadamu kupamba na hata kutunga. Hii mara nyingi husababishwa na kuwa na shauku kubwa au kuwa na imani thabiti. Kwa hivyo, tunapaswa kupima kila kitu kinachowasilishwa kwetu kwa uangalifu sana, lakini tubaki tayari na rahisi kubadilika na tuwe tayari kurekebisha maoni yetu, ikiwa ni muhimu kufanya hivyo.

Hapa ni Mabwana wa Mwanga.

Kuna Viumbe wengi katika Ngazi za Juu za Kiroho, Wote Wakiwa na lengo na misheni zao tofauti, wanafanya kazi peke Yao au kama Kikundi.

Kama unavyoweza kufikiria, kuna kazi nyingi za kuzingatia wakati uko katika msimamo Wetu.

Ukiangalia Dunia na tofauti zake zote, huwezi kumpa kila mtu mafundisho sawa. Fikiria dini zote tofauti ulimwenguni leo, na kila dini imegawanyika katika imani tofauti pia.

Nia ya kuchukua mwili wa kibinadamu ni kwa namna fulani, wakati bado uko hai, kutafuta njia yako kurudi kwenye Chanzo (Mungu). Jinsi unavyofanya hii inategemea sana mahali unapoishi, jinsi ulivyolelewa, imani yako na kadhalika. Watu watavutiwa na aina tofauti za mafundisho.

Mara tu mtu anapoanzishwa kwenye Mwanga na Sauti basi anaweza kufuata Ukweli wao kurudi kwenye Chanzo. Wana uwezo wa kupata Upendo, Amani na Utulivu zaidi ya kitu chochote ambacho wamewahi kufikiria au kuota. Lakini sio kila mtu atataka hii; watazingatia na kufikiria kuwa labda Meditation ni ya kuchosha, kutosisimua au ya ajabu (weird). Mtu anayefanya meditation anaweza, na anayo, na bado, anafuraha Ulimwenguni. Tofauti ni kwamba wana mahali pa kuweka nanga wakati mambo yanapokuwa magumu. Wanaweza pia kuona maisha kutoka kwenye mtazamo tofauti na kuwa na busara zaidi.

Kazi yetu katika Ngazi za Juu za Kiroho ni kujaribu kusaidia watu kufikia uwezo wao wa hali ya juu wakati wakiwa kwenye umbo la kibinadamu. Jinsi tunavyofanya ni kutoa mafundisho tofauti kwa matumaini kwamba watu watafanikisha hii.

Kusudi la msingi la maisha yoyote ni Kupenda na Kujifunza. “Utajiri” wa maisha ya mtu kweli unategemea na uelewa kamili, wa sababu hii.

Mfano wa gorofa ndefu unaonyesha mwelekeo kutoka kwenye ugumu hadi urahisi jinsi tunavyopanda kwenye gorofa au sakafu za juu. Ndiyo ilivyo pia kuwa, wakati mtu anapoanza kufanya meditation kwenye Nishati ya Mwanga na Sauti ya Kiroho, wanajua, ”wanaona” wingi wa rangi, maumbo na miundo. Sauti kawaida husikika kama mchanganyiko wa masafa kadhaa. Hata hivyo, kadri mtu anayefanya meditation anavyoendelea kwenye Njia Meditation zake kwa ujumla zitakuwa rahisi zaidi. Rangi zitakuwa safi nyeupe au Dhahabu Nyeupe, wakati Sauti zinakuwa nzuri, za juu kwa masafa, sare zaidi na pana.
Mwishowe, wakati unapopata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment Mtu anayefanya meditation anapaswa Kuvuka Mwanga na Sauti na kutokomea kabisa kwenye Umoja.

Hii inapaswa kuwa kielelezo cha mwisho cha urahisi au (simplicity)!