Uwezekano wa kweli wa Ubongo wa Binadamu

 

Ubongo unabakia kuwa moja ya siri yetu kuu; wote tunao mmoja na bado tunafahamu kidogo jinsi unavyofanya kazi. Katika miongo michache iliyopita sayansi imefanya uvumbuzi mkubwa wa kineourologia na neva na inaweza kufuatilia mawimbi ya ubongo pamoja na maeneo yenye shughuli wakati wa mchakato wa mawazo.

Ambacho hakijulikani ni asili ya kweli ya kufikiri, mtazamo na kumbukumbu pamoja na maelezo ya kukubalika ya mambo kama kuwa nje ya mwili na uzoefu wa karibu na kifo. Pia kuna dhana nyingi na mjadala wa kama, kweli, tunatumia ubongo wetu kwa uwezo kamili.
(Tafadhali sisi hatumaanishi nadharia ya 10%)

Ni hatua hii ya mwisho ambayo tunataka kuishughulikia katika makala hii. Kila sehemu ya mwili wa binadamu ina kazi inayojulikana vizuri kabisa, hata ‟appendix” kihistoria, ilikuwa na matumizi muhimu. Hivyo kwa nini tuna ubongo ambao unaonekana kuwa zaidi ya vile sisi tunavyoutumia kwa kawaida?

Wakati wa kuandika (2016) sayansi iko ukingoni kwenye ugunduzi wa kuwepo kwa ‟Dimensions” zingine kwa kutokana na majaribio yaliyofanywa na CERN. Kwa hilo, tuna maana kama hali halisi, na sio mbinu tu ya hisabati ambayo husaidia kuthibitisha nadharia ngumu ya kosmolojia.

Tunajua pia kwamba idadi kubwa ya watu kote duniani wote wanakuwa na ndoto kuhusu Viumbe wa Mwanga. Hivyo kama tukiweka mawazo haya pamoja, hitimisho dhahiri ni kwamba kuna Ulimwengu wenye ‟Dimensions” mbalimbali ambazo zina Akili au ‟Intelligence”.

Hii basi inaturudisha kwenye ubongo na kushirikisha na kuutumia kwa uwezo wake kamili. Je inawezekana kwamba kuna sehemu yake, au kuna utaratibu ndani yake kuwa ipo katika nafasi ya kuwa na ufahamu wa ‟Dimensions” hizi nyingine zaidi, na kuwasiliana na kile kilichopo huko?

Wale ambao mnatahajudi kwenye Mwanga na Sauti tayari mnajua jibu. Tunaweza kuwepo zaidi ya mawazo yetu na kuwa na ufahamu kamili wa ngazi hizo kubwa ambazo kwa kawaida tunaziita kama ngazi za Kiroho. Wengi wenu pia mnafahamu viumbe au ‟Intelligence” ambao wako kwenye kanda hizi. (tazama makala kuhusu Miungu, Waokozi na Uongozi).

Hatimaye, sisi tunapendekeza kuwa kuna masuala mengi ya ubongo, ambayo hakika hatuyajui, na kwamba sehemu hizi za ubongo zipo ili tuweze kuzitumia kuingia kwenye ngazi hizi za juu au ufahamu wa juu, zaidi ya mipaka ya ulimwengu wa 3-D.

Huu ni mlango kwa Evolution yetu ya Kiroho.

Kutoka Uongozi:

Kuhusiana na ubongo na kazi yake – hautumiki kikamilifu na sababu ni kuwa tangu Binadamu amekuwa Duniani kumekuwa na mabadiliko makubwa jinsi ambavyo umetumika.

Tangu binadamu alivyoiishi katika hali ya kale mpaka sasa kumekuwa na mabadiliko mengi na ubongo umelazimika kubadilika na kukabiliana na mabadiliko haya. Sisi ni tunazungumzia juu ya kupanda na kuanguka kwa ustaarabu, na Ufahamu wa Kiroho ulicheza sehemu kubwa. Kwa hiyo, bila shaka sehemu hiyo ya ubongo inayounganisha na ngazi za juu ulitumika mpaka kuanguka na kuharibika kwa ustaarabu fulani. Kisha ukalala bila kutumika.

Tunadokeza kwamba, kila ustaarabu mkubwa imehusisha kwa namna fulani, kwa kiwango kikubwa au kidogo Ufahamu wa Kiroho.