Ushuhuda (J. H.)

 

Nilitahajudi usiku kucha, Jumapili, kwa mara ya kwanza kwangu lakini hapakuwa na wakati, ilikuwa rahisi bila kujitahidi na ajabu. Mimi daima nilihisi kulikuwa na safari, mahali papya na kusisimua, mahali fulani ninapoweza kuridhika milele.

Ghafla, papo hapo hapakuwa.

Kila kitu kilisimama – hakuna Sauti – hakuna Mwanga – hakuna Kitu,
Ile sehemu yangu tu ambayo ilikuwa pamoja na kile ambacho sio Kitu, “Mimi” nilikuwa sio Kitu.
Nilikuwa kila Kitu, nilikuwa chanzo cha sio Kitu na kila Kitu, maneno ni duni kiasi hicho, lakini ilikuwa nzuri na kile ninachoweza kulinganisha nacho ni UPENDO.

Kila Kitu na hakuna Kitu, vurugu la maneno, lakini ni wazi kama mchana kwangu mimi, ya kupendeza na bado sio. Mimi nimeacha na kusimama kila baada ya muda lakini naweza kuendelea, ni rahisi na mimi nimepewa nguvu, nimehusishwa na kila Kitu na kile ambacho sio Kitu, mimi naimba??

Nilihisi kama ulimwengu wangu umekuwa ‟imploded”, mimi sikuwa nakwenda mahali popote, haikuwa safari, upanuzi wangu hauna mwisho, ‘Mimi’ nilikuwa safari, hakukuwa na kitu, NILIJUA – NILIELEWA kile nilichokuwa natafuta – kwa miaka 20 na bila kujua mwenyewe nilikuwa kizuizi, unyenyekevu mkubwa, tunachohitaji ni UPENDO, sio upendo wa duniani wa kimwili, lakini upendo wa dunia (global love) ambao unaweza kuponya mataifa.

Kwa hiyo mimi najaribu kujishusha na kujiweka imara duniani ili niweze kufanya kazi, pamoja na kwamba sina hamu yeyote ile!