Kutuama na Utulivu wa ndani unatuongoza kwenda kwenye Hali ya mabadiliko makubwa ambapo hakuna kitu kinachohitajika na hakuna hamu ya kutaka chochote. Sisi tunatambua kuwa huru tu.
Akili na mwili havitahajudi wala havipati Enlightenment. Kile ambacho ni Wewe (Self) kinajitabua Chenyewe na kutokana na kutambua huku elimu ya kweli hushushwa kwenye mwili.
Utambuzi wa Mungu ni lengo Kuu la Mwisho kwani akili haiwezi kuelewa utambuzi huu. Hakuna mwanzo wala mwisho. Ni zaidi ya kuzaliwa na kufa. Unajihisi Kuwa kila mahali na wakati na nafasi hutoweka. Ni Neema na Furaha ya juu kuliko zote na Uvuvio ambao unafutilia mbali dhana zote.
Enlightenment hupatikana papo hapo wakati hakuna matumaini yoyote. Enlightenment ni utambuzi wa kweli wa Binafsi (Self), ni Nafsi / Kiini (Soul / Essence) ambayo ilipoteza utambulisho wake na inatambua uwepo wake kila mahali na katika kila kitu.
Mimi nimetambua Ukamilifu wangu, Uwepo wangu Kamili katika kila kitu na wakati wote. Ni Faraja na neema kubwa zaidi kuliko ya kufa na kuzaliwa. Ni hali ambayo Roho/Nafsi (Soul) yako inafunuliwa Kwako na kufunuliwa kwa maeneo mengi yasiyo na kikomo na mng’ao wa ajabu na Kiini cha kweli cha kudhihirika kwetu.
Enlightenment sio maarifa na mafanikio. Akili ndiyo inapambana kujifunza, kutafuta, kupata, kufikia, tamaa na kutafuta. Hii ndiyo sababu akili kamwe huitahajudi wala kuwa Enlightened. Enlightenment ni kuwa. Tahajudi bora inaonekana wakati tunajisalimisha na kuruhusu sisi wenyewe Kuwa na kuacha kila kitu Kuwa. Kisha bila kutarajia mtu anajitambua Binafsi. Ni zaidi ya mawazo.
Miili yetu wala akili zetu hazitahajudi na kupata Enlightenment. Ni nafsi yetu ambayo inajitambua yenyewe, ni Nafsi / Kiini (Soul / Essence) yetu ambayo inakuwa Enlightened. Ni utambuzi wa Mungu.
Maarifa ni mipaka. Maarifa ya kweli yanafunuliwa au kushushwa kwa mwili wakati sisi tunapovuka mipaka na kujisalimisha kwetu wakati tunajikuta huru bila mipaka na kuwa mmoja na kila kitu.
Asante kwa uongozi wenu na Ningependa kuwashukuru Uongozi wa Kiroho kwa Neema. Najua haikadiriki. Njia nzuri ni kuwahudumia wengine na kuongoza wengine katika safari hii ya ajabu. Inawezekana na inapatikana kwetu wote.