Chanzo Cha Maarifa Yote

 

Yanatoka wapi mawazo mapya, ugunduzi na uvumbuzi?

Watu wengi wengedai kwamba yametoka kwenye akili zao wenyewe na walipata uvuvio na kuongozwa na baadhi ya tukio, uchunguzi au hata ndoto. Je, tunawazaje kueleza kuhusu watoto maalum wenye akili na uwezo wa kuandika ‟symphonies” au kuzungumza lugha nyingi au wenye uwezo mkubwa wa hisabati? Wengi wangedai na kupendekeza watoto hawa maalum wamezaliwa na vipaji vyao vikiwa tayari vimepandikizwa kijenetiki ‟genetically” mwilini. Je tunawezaje kueleza ukweli ambao unajulikana kuwa kwa wakati mmoja wakati mwanasayansi mmoja akiwa anafanya kazi ya ugunduzi mpya mahali fulani, kuna wanasayansi wengine katika maeneo mengine ya dunia wanaofanya utafiti kama huohuo; ushindani daima uko kwamba nani atachapisha au kupatenti kwanza. Je, tunawezaje kueleza tukio la kumfundisha mnyama hila katika sehemu moja ya dunia, na ikawa rahisi kuwafundisha wanyama wengine wa aina hiyo mahali pengine na wao wakajifunza kwa haraka zaidi?

Hivi karibuni tulipata habari inayotoa mwanga mpya kabisa juu ya maswali hayo hapo juu. Tumeambiwa kuwa wanadamu ni kama redio, kamili na antena, ambayo unaweza ku‟tune” kwenye vituo mbalimbali. Mawazo mapya, maongozi na uvumbuzi yanatoka ngazi za juu za maumbile: na sisi tunaweza kuwa na uwezo au kutokuwa na uwezo wa ku‟tune” na kuchukua taarifa zilizopo. Zinatolewa wakati watu wamebadilika kiasi cha kutosha na inaonekana kuja katika mawimbi (tazama makala ya Mawimbi na Mizunguko). Mtu mmoja anapokuwa ‟tuned”, mfereji wa ubadilishanaji unakuwa mpana zaidi, hivyo inakuwa rahisi kwa wengine ku‟tune” na kusikiliza. Hii pia inahusu wanyama na inaelezea jinsi ambavyo hila inaweza kufundishika kwa urahisi zaidi.

Sisi kama watahajudi labda zaidi tuna uwezo wa kuleta chini ‟realizations” na Ukweli wa Kiroho. Kama sisi tunasema kwa uhuru, au kuandika kuhusu matokeo yetu, basi sisi pia tutakuwa tunajenga na kupanua mifereji ili wengine waweze kugundua na kugeuzwa. Hii inatumika kwa teknolojia inayotumika kwa madawa ya matibabu na mradi EMF. Kwa kushusha chini na kuleta habari hizi na kuziweka wazi kwa wote, inafanya kuwa rahisi kwa watu wengi, ambao baadhi yao wataweza kuendeleza mawazo hayo zaidi. Wakati huo huo mawazo ya watu katika sayari yatabadilika na inawaunganisha, ili waweze kuwa na uwezo zaidi wa kupokea teknolojia mpya
.

Maarifa ya Kweli daima yamekuwa yakipokelewa kwa njia hii.