Kuwa Kwenye ‟Moment”

 

Hili ni somo ambalo mengi tayari yameandikwa na watu wengi wanadhani wanalielewa. Hata hivyo, kwa sababu litakuwa msaada kwenye kutahajudi, ni muhimu kuchunguzwa na kutekelezwa katika maisha ya mtu.

Kwa maana nyingine ni vigumu kutokuwa katika wakati huu. Wewe, ama una ukufahamu wa kile unachofanya kwa sasa, una ufahamu wa mawazo yanayohusu awali yaliyopita au una ufahamu wa mwelekezo katika siku zijazo. Kile ambcho usemi huu unamaanisha ni sawa na dhana ya kutahajudi, maana yake ni “mkusanyiko kwenye lengo moja kwa muda mrefu.” Hivyo kuwa kwenye ‟moment”, ni kuwa na uwezo wa makini wa mkusanyiko ‟focus” kwa muda mrefu kwenye mada moja au tukio. Tukio hili linaweza kuwa linafanyika wakati wa mkusanyiko wa lengo au kuwa mfululizo wa mawazo ambayo ni zamani au baadaye. Jambo la muhimu ni kwamba usiruke toka kwenye mfululizo mmoja wa mawazo na kwenda kwenye mfululizo mwingine wa mawazo. Hii huelekea kutokea wakati una stresi, wakati majadiliano yako ya mawazo mara kwa mara hukimbia na kuzunguka katika duara, mara nyingi bila kufikia hitimisho na uamuzi thabiti.

Kinachotakiwa ni kuwa na nidhamu: kuwa na uwezo wa kuchagua kazi fulani au mada na kisha kuzingatia kabisa na mkusanyiko wako wote, mpaka matokeo au hitimisho linafikiwa. Katika hatua hii ngazi za stresi zitapungua na wewe utakuwa huru kuondoa hoja hiyo kwenye orodha yako akilini. Hii ni njia ya ufanisi sana kuishi na inakupa muda mwingi, kukuwezesha wewe kuwa ‟spontaneous” zaidi. Kama tunaweza kusafisha “trei” letu, basi sisi tuko tayari kukabiliana na kazi nyingine mara moja. Mizigo ambayo tunabeba daima inawekwa kwenye kiwango cha chini na tunakuwa huru na uwezo wa kushiriki sasa hivi.

Wakati ukikaa na kutahajudi, akili yako itakuwa wazi na mkusanyiko makini kwenye pumzi yako, mantra au baada ya Kuanzishwa kwenye Mwanga na Sauti. Huwezi kukalishwa hapo na kutengeneza orodha ya mambo ya lazima kufanya na wasiwasi kuhusu wakati na jinsi ya kuyafanya.

Ushauri huu ni rahisi kutoa lakini unaweza kuwa vigumu kuutekeleza. Anza kwa kuchukua kazi moja na kuifanya hadi kufikia mwisho, kwa mfano, wakati barua au barua pepe inapofika, tatua mara moja na tenda kila kitu kinachoihusu mara moja (kama inawezekana). Wakati unafanya kitu kwa vitendo, bila kujali ni cha kawaida, jaribu kuwa makini na kazi unayoifanya badala ya kuchukuliwa na mawazo mengine yasiyohusiana na kazi hiyo. Utaona kuwa unakamilisha kazi bora zaidi, na kwa muda mfupi na utashangaa huenda hata utafurahia! Kwa namna nyingine ni kama kurudi kuwa kama mtoto tena, wakati kila kitu kinachokuzunguka kilipokuwa kipya na cha kusisimua.

Kwa kufanya mazoezi na mbinu hii, utaanza kuvuna matunda duniani, kwa kuendeleza usimamizi bora wa wakati, kupunguza viwango vya stresi na dhiki kwako na matokeo yake kufurahia zaidi sana, tahajudi zenye lengo na kutimiza.