Ushuhuda (D.H.)

 

Tahajudi ya mwanga na sauti ni njia ya kale ya kutahajudi ambayo inafunua na inaonyesha njia ya kiroho kutoka ufunuo wa lotus ya petal elfu moja hadi Enlightenment. Kuona lotus ya petal elfu moja kwenye Initiation yangu ya kwanza nilipokuwa na umri wa miaka 20 mnamo mwezi Februari mwaka 1987 ilikuwa ni uzoefu wa ajabu wa Kiroho ambao ulinionyesha jinsi gani ngazi za kiroho za ndani ni safi. Kuendelea kupitia initiations zaidi kadri miaka ilivyopita kulithibitika safari ya ajabu ya ufunuzi wa kiroho wakati nguvu za mwanga na sauti zilizidi kuwa ‟suble” na safi mpaka nilipopokea nguvu kwa ajili ya Enlightenment mnamo Juni 2006.

Tahajudi ya mwanga na sauti imenifunulia kielelezo na Usafi wa UPENDO kwenye Enlightenment. Upendo unaounganisha uumbaji na kujaa kwenye kiini chake, na ni kitu mbali zaidi ya kile ambacho unaweza kuwa na uzoefu nacho siku hadi siku kwenye maisha na zaidi ya kile ambacho akili inaweza kuelewa.

Baada ya Enlightenment, licha ukubwa wa hali ya ufahamu, mtu anatambua kwamba huu ni mwanzo mwingine tu, na ni fursa mpya kwa ajili ya ukuaji na kutumikia wengine wakati tuna mwili na maisha ya kuishi katika dunia.

Kwa sasa Uongozi wa Kiroho Wanafanya kazi na wale ambao walishakuwa na Ininitiation ya 3 au Enlightenment kuleta uwazi zaidi wa ufahamu na kutuendeleza Kiroho zaidi ya kile ambacho tulidhani kuwa kinawezekana, na maarifa haya tunataka kuwapa na kushirikisha wale wote ambao wanataka kujifunza kuhusu hivi ‟vito” vya kiroho. Hivyo safari haisimami au kwisha hadi siku ya kufa na kisha safari mpya inaanza.

Inabidi kutoa heshima kamili kuhusu maendeleo yangu ya kiroho hadi Enlightenment, kwa kuwa na Mwalimu wa Kiroho na kufanya kazi kwa njia ya Uongozi wa Kiroho, ambao Wameweza kutoa Hali hizi za ufahamu, na kwa watu walionijali kwa kiasi cha kutosha kunisaidia mimi wakati maisha yananirushia changamoto zake kubwa. Kusema mimi nimekamilisha safari peke yangu bila neema ya kiroho kila siku na misaada kwa miaka mingi itakuwa ni kudhoofisha ukubwa na umuhimu wa yale niliyopata kupitia kwa watu wengine.

Mnamo mwaka 2015 Uongozi wa Kiroho Wanatoa moja kwa moja neema kwa initiations hizi pamoja na Enlightenment. Kile ambacho kinahitajika ni hamu ya kweli ya kutahajudi kwenye mwanga na sauti na kutoa kitu kizuri duniani kwa njia yako mwenyewe bila kutaka kutambuliwa au kuzawadiwa. Enlightenment haijawahi tena kuwa rahisi au kupatikana kwa urahisi zaidi kwa Mtafutaji wa dhati wa ukweli.