Sababu ya Kuwepo kwako

 

Tumeandika juu kwenye Tovuti ya Nyumbani, ‟Fanya Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho “Enlightenment” kuwa Lengo lako: ndio Sababu ya Kuwepo kwako.”

Tunahisi taarifa hii inastahili ufafanuzi. Kufikia Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho ni wazi kuwa ni tukio la nadra na kwa hivyo inapendekeza kuwa idadi kubwa ya watu hushindwa kutimiza sababu ya wao kuwa kwenye mwili. Watu wengi hawaonyeshi nia ya kutafuta njia hiyo na bado wanaweza kuwa maisha kamili, ya maana ambayo wanaonyesha maadili ya kiroho.

Uelewa wa kweli wa kauli unahusisha Kiini ambacho Roho binafsi zinajitokeza. Ni Kiini ambacho kimetengenezwa kutoka kwa Umoja (Mungu) na kinatafuta Ukombozi. Kina tamaa na hamu ya kurudi na kuchanganyika na Umoja ambapo ndipo kilipotoka. Ni tone la mvua linalotafuta Bahari isiyo na mwisho.

Ili kukamilisha hili, Kiini kinazituma Roho ambazo zinajitokeza kwenye maumbile ya ngazi za chini kama watu binafsi, kama wewe na mimi. Tunakuja kujifunza masomo ya maisha. Mchakato huu hauna mwisho- tunaambiwa unaendelea hata baada ya kifo cha mwili!

Wakati fulani wa maisha Roho inaweza kuvutiwa kufuata njia ya kiroho. Si njia zote zinaelekea kwenye Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho. Hivyo Mtafutaji lazima kubagua sana na kuangalia kwamba njia aliochagua itamfunulia kwa ukamilifu Umoja Kamili kama Ukweli halisi, sio imani tu au mafundisho.

Sisi tunasema kuwa Njia hii inakuongoza kuelekea kwenye Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho wa Kweli na kuthibitisha madai haya kwa kutoa shuhuda za idadi kubwa ya Watahajudi waliofikia huu Hali ya Mwisho. Unaweza kuwasiliana na watu hawa na pia kukutana nao. Unakaribishwa kuuliza maswali yoyote; tunaahidi kuyajibu kwa uaminifu. Kama hatuna jibu basi tutasema hivyo.

Kwa vile tuna mawiliano moja kwa moja na Uongozi wa Kiroho tunaweza kutafuta jibu kutoka Kwao na kukujulisha baadaye. Kwa ujumla tutafanya hivyo kwa kuweka jibu kwenye makala ili wasomaji wetu wote wanufaike na habari hiyo.

Tunatumaini hii itasaidia kufafanua kauli hiyo hapo juu.