Kujitambua Mweyewe na Kumtambua Mungu

 

Kujitambua Binafsi na Kumtambua Mungu ni tofauti kabisa. Kuna fafanuzi nyingi zinazopatikana kwenye maandishi ya kiroho, mengi ambayo yana utata na hata kuwa kinyume. Kwa sababu hiyo sisi tuliona tunapaswa kujaribu kuweka wazi maana ya maneno haya.

Kujitambua Mwenyewe

Hii hutokea wakati tunapopata uzoefu wa upanuzi wa Ufahamu ambao tunatambua ya kwamba kila kitu tunachofahamu ni nafsi zetu. Tunahusiana na yote tunayofahamu: maumbo, sauti na hata nafasi. Kila kitu kinaonekana kipya kabisa na ni Nishati ambayo ni sisi!

Hii inaweza kutokea kwenye maisha ya kawaida. Mara tuko na fahamu zetu na tumefungwa kwenye miili yetu midogo na ghafla tunakuwa kila kitu katika mazingira yetu yote – na yote kwa wakati mmoja. Kwa kawaida hii inasababishwa na akili au hisia kali au vyote pamoja. Mtu anaweza kuwa ana furaha sana au katika kina cha kukata tamaa sana; inaonekana kufanya kazi kama vali ya usalama.

Kwa wale ambao Wanatahajudi kwenye Nguvu za Kiroho Kujitambua Binafsi kunaweza kutokea katika ngazi za Juu sana na kuwa na kina kikubwa. Tukiwa kwenye Tahajudi ya kina kirefu tunaweza kuwa na uzoefu wa kuunganika na Mwanga na Sauti, na kujua kwamba sisi Ni hizi Nguvu – na sio watazamaji tena.

Kumtambua Mungu

Hii inaweza kutokea wakati Unatahajudi kwenye Mwanga na Sauti ya Kiroho. Kwa njia ya Neema ya Mwalimu ‟Master” (au moja kwa moja kutoka Uongozi wa Kiroho) kuna uwezekano wa Mtahajudi kuvuka Nguvu zote za maumbile. Nguvu Hizi ni matokeo, na Chanzo ni (Mungu), Zenyewe sio Chanzo. Zenyewe ni kielelezo cha uwili (‟duality”) ambapo kuna mipaka.

Chanzo cha kila kitu ni Umoja tu, Kiini ambacho Kipo tu.

Unapofikia Kumtambua Mungu au Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho wa Kweli, Ufahamu wa Kuwa Usio na Mwisho, Mtahajudi atakuwa na utambuzi ‟realizations” nyingi ambazo zimefugwa kwenye mawazo.

Kwenye Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho wa Kweli:

  • Hakuna Mwanga, hakuna rangi, hakuna sura au umbo.
  • Hakuna Sauti au mitikisiko ‟vibrations”.
  • Hakuna binafsi; hisia za kuwa binafsi na kujitenga hutoweka kabisa.
  • Hakuna eneo; hakuna mbele, nyuma, kushoto, kulia, juu au chini.
  • Hakuna mipaka, kingo au vikwazo.
  • Hakuna muda, zamani au sasa, au baadaye kwa sababu hakuna mabadiliko.

Njia bora ya kuzungumza kuhusu ‟Enlightenment” ni kueleza kile ambacho ‟Enlightenment” sio. Kama sisi tungeweza kuipa ‟Enlightenment” ubora, basi neno peke yake ambalo tungeweza kutumia lingekuwa UPENDO. Hii isije kuchanganywa na upendo wa kidunia lakini Upendo kabisa bila masharti na Umoja au Chanzo cha Uumbaji na Maumbile yote.