‟Ascension” Imeanza

 

Tunafahamu kutoka Uongozi wa Kiroho kwamba Kupanda ‟Ascension” haitakuwa tukio la janga lakini litakua na mchakato taratibu na wa upole.

Kadiri watu zaidi na zaidi wanavyoanzishwa Nguvu za Mwanga na Sauti itaanza kuwa na athari nzuri itaongezaka kwenye Sayari hii pamoja na wakazi wake. Mchakato huu tayari umeanza na kuna dalili nyingi zinazoonyesha hili.

Tayari tumetaja kwamba watu wengi Duniani wanakuwa na ufahamu wa Sauti za juu. Wengi wanafikiria ni kawaida na kila mtu anajua; wengine wanafikiri ni hali ya matibabu kama vile ”tinnitus”! Ukweli ni kwamba watu wanaendelea kuwa nyeti zaidi na “wanasikia” kwa njia tofauti. Sauti ambazo tunazizungumzia hazisikiki kwa masikio ya kimwili. Ni kana kwamba imepatikana hisia nyingine! Hii ni mtiririko wa Sauti ambayo Watahajudi wenye uzoefu wanaiongelea na iko kwenye kumbukumbu vizuri kwenye vitabu vya Kiroho. Jambo la kushangaza ni kuwa idadi kubwa ya watu wanaoripoti matukio haya hawajawahi kutahajudi katika maisha yao.

Baadhi ya watu wanakuwa na ufahamu wa Mwanga. Hii kwa kawaida huchukua mfumo wa maumbo ya kijiometri na rangi. Sio ya asili kimwili; huonekana wakati mtu akiwa macho kikamilifu na wakati amefunga macho hasa wakiwa kwenye chumba chenye giza. Si aina ya kuota ‟daydreaming” au kuundwa kwa kutumia mawazo ‟imagination”. Wale wanaoshuhudia Nguvu hii wanasema ina ubora wa kuwa na kinga na Upendo. Watu ambao huona Mwanga pia husikia Sauti.

Asili ‟Nature” inakuwa kama “inaamka”. Watu wanasikia ‟Ndege wakiimba” zaidi mwaka huu na inaonekana kwa sauti kubwa zaidi na zaidi mara kwa mara. Kama ni ndege wanaobadilika au kama ni watu wanaendelea kuwa nyeti na hisia zaidi hatuna uhakika. Tunachojua ni kwamba jambo hili limeripotiwa kutoka pande zote Duniani kuanzia mapema mwaka 2017.

Sehemu nyingine ya mabadiliko inaonekana kuwa inatokea wakati wa usingizi. Watu wanaripoti kuwa na ndoto nzuri zaidi na wazi kiasi kwamba inakuwa kama wako kwenye maisha sambamba na haya waliyo nayo. Huu au hizi ulimwengu mbadala ni kama kweli kama hii ya Duniani. Wakati mandhari kwa kiasi ni ya kawaida jinsi muda unavyopita pamoja na sheria za fizikia ni tofauti kabisa.

Mengi ya matukio yaliotajwa hapo juu hutokea kwa vijana, ambao wengi wao ni umri wa kuanzia miaka kumi na tatu hadi kumi na tisa. Wao wanakabiliwa na matatizo ya kejeli toka kwa wenzao na/au kuitwa watu waajabu na kuwekwa chini ya uangalizi wa madaktari wa akili na wazazi wao. Kwa sababu hizi wao hukaa kimya bila kumwambia mtu yeyote. Ni muhimu kwamba tunawahimiza kuzungumza. Sisi kama Watahajudi wa Mwanga na Sound tunajua kwamba Ulimwengu umejaa Maajabu na tunaweza kuwahamasisha wale walio karibu yetu kuzungumza kuhusu Ukweli.

Uongozi wa Kiroho wametuambia kuwa ‟Ascension” italeta unyeti zaidi ambayo utasaidia kuongeza maelewano kati ya wakazi wa Sayari hii. Hasa vizazi vipya vitakuwa “vinaamka” kwa mabadiliko haya na kuwa na Fahamu zaidi; hatma ya dunia hatimaye itakuwa katika mikono yao.