Ushuhuda

 

Wakati mimi nilipokaa kwa ajili ya ‟Initiation” yangu nilikuwa na matarajio kidogo sana. Ingawa nilikuwa na heshima kwa watu ambao walinifundishwa na kuniongoza nilihisi kuwa, kutokana na bidii yao, wangekuwa na uwezekano wa ‟kutia chumvi” kidogo.
 

Nilikuwa nimekosea kabisa! Hakuna kitu ambacho kingeweza kunitayarisha kwa kile kilichotokea wakati mimi “nilipoguswa”.
 

Nilirushwa na kuchukuliwa na kupita kwenye ngazi nyingi za Mwanga ambazo zilifunua jiometria zilizoonyesha uzuri kabisa na ukamilifu. Hisia zangu zilizidiwa na akili yangu ikajua mara moja jinsi ilivyokuwa ndogo na sio kitu.
 

Hakuna chochote katika dunia hii cha kulinganishwa na utukufu mkubwa na ukamili wa ngazi hizi za maumbile. Haiwezekani hata kupata maneno ambayo hufikia karibu ya kuelezea ngazi hizi. Nilichotaka kufanya ilikuwa ni kufa. Ingawaje nilikuwa na maisha ya ajabu hapa Duniani kama ningepewa uchaguzi mimi kamwe nisingerudi. Ilikuwa kweli ni ajabu kiasi hicho!
 

Niliporudi sikuweza kuongea kwa muda wa nusu saa na mwili wangu wote ulikuwa unatetemeka, sio kutokana na hofu ila mshtuko wa kushuhudia kitu ambacho ni zaidi ya uwezekano wa mawazo yote.
 

Upendo niliopata uzoefu wake siku ile ulibadilisha maisha yangu milele; nilijisikia kulia tu!