Mwaka mmoja uliopita kwenye mwezi wa Agosti Nilipata ‟Enlightenment” kwa njia ya fadhila na Neema ya Uongozi wa Kiroho. Nilianza kuwa na udadisi wa kutafuta Ukweli kuhusu asili yangu na maumbile nikiwa na umri wa miaka 7. Nilipokuwa na umri wa miaka 21 nilipata Neema ‟Grace” na kuanzishwa ‟Initiated” kwenye Mwanga na Sauti ya Kiroho.
Mabadiliko makubwa katika ufahamu wa mwanadamu na sayari kwa ujumla inabidi yatokee kuleta uwiano wa ‟Spirit” na ‟Matter”. Hiki ni kipindi ambapo ulimwengu unatoka kwenye giza kwenda kwenye nuru na mchakato huu ulianza muda mrefu uliyopita na kudhihirishwa na kufunuliwa kwa baadhi ya watu wa Kiroho waliokuwa wanyenyekevu na kuupokea mnamo mwaka 2015.
Kwa Wakati huu muhimu mnamo Februari 2015 nikiwa sifahamu kuhusu njia mpya ya ‟Lightwave”, nilichukuliwa Kiroho kwa njia ya kutahajudi na Kiumbe wa Uongozi wa Kiroho na kushuhudia kile ambacho mimi nitakiita MJI WA MWANGA WA DHAHABU. Katika ngazi hizi Niliona idadi kubwa ya Viumbe wa Mwanga wakifanya kazi katika maagizo na mipango fulani ambayo haiwezi kuelezwa kwa akili kwa ajili ya kuongeza ufahamu wa dunia hii kama maandalizi ya ‟Ascension”. Mtazamo mzima na mandhari katika ugunduzi huu ilikuwa kama Viumbe wakifanya kazi katika ‟universal” supa kompyuta ambayo hudhibiti ufahamu wa maumbile na ndani na nje ya ‟Matrix” kwa njia inayonekana kuwa mchanganyiko rahisi wa Hesabu za ‟Matrix” na Jiometri za ajabu zisizodhaniwa.
Kwangu mimi ilikuwa ni kama aina ya kusafiri kwenye ‟space” katika malimwengu ‟universes” nyingi. Niliona na kutambua kuwa Malimwengu yote yameingiliana katika njia ambayo ni siri kwa akili na sisi tunatoka kutoka mzunguko mmoja wa hali halisi kwenda sehemu nyingine ya ulimwengu mwingine kwa muda ambao ni chini ya sekunde toka ulimwengu hadi ulimwengu.
Uzoefu huu ulihakikiwa kwenye “Enlightenment” yangu (baada ya mimi kuunganishwa na “Lightwave”) baada ya kujua kuwa kulikuwa aina mbalimbali za Mimi katika Malimwengu haya yote zilizopo wakati huo huo na sambamba. Nilitambua miaka bilioni moja iliyopita na miaka bilioni moja ijayo zote zipo milele kwenye sasa isiyo na Muda au wakati. Na Kile ambacho Si Chochote kina kasi zaidi kuliko kile kilichoko kila mahali kwani kasi kamili ni utulivu kamili.
Aina hii ya uvumbuzi iliniacha kwenye hofu na ajabu, na mimi nikawa kimya sikuongea kwa muda mrefu sana. Nakumbuka wakati nilikuwa na nia ndani ya moyo wangu kutembea Njia ya Mwanga wa kweli wa kugundua siri ya Kuwepo.
Moja ya Uzoefu wa ajabu kwa Kupitia Uongozi wa Viumbe mnamo Mei 2016 ilikuwa kugundua siri ya Muda, mchakato wa maumbile na kile mtu wa kawaida anachokiita KIFO. Kwenye tahajudi moja nilisafiri kwenye Sauti ya Kiroho na Mwanga wa Kiroho na kutambua utupu. Niligundua kwamba Kuwa kwangu ni zaidi ya aina zote za maumbo na kwamba utupu na hali ya utupu ni Hali ambayo hakuna siri zilizojificha, lakini hakuna kitu kinaweza kupatikana katika sasa ya milele.
Nilitambua Sijawahi kuzaliwa, na mimi kamwe sitakufa kwani mimi nilikuwa Kiumbe asiye na umbo! Nilijua kile kinachokuja na kwenda kama kuzaliwa na vifo ni udanganyifu tu ulioundwa na fahamu katika ngazi mbalimbali za maumbile kama ‟Mchezo Takatifu wa Mungu”. Hii ilikuwa ni kipindi kikubwa cha mabadiliko ya Uelewa Wangu. Suala la kuwa mimi ni nani lilijibiwa kwa njia ambayo haiwezi kuelezwa kwa maana yoyote ya kibinafsi. Mimi bado ninatafakari na kwa unyenyekevu kujifunza kutoka kwenye Maarifa ya ngazi za juu.
‟Realizations” ya hali ya utupu ‟formlessness” na tupu ‟void” ulifanya mimi kufahamu sehemu ya ajabu ya jiometri ya ufahamu na jinsi maumbile yanaumbwa kama Maonyesho na kielelezo kamili cha Mwanga wa Kiroho na Sauti ya Kiroho. Hizi ‟Realizations” zilikuja kama sehemu ya kuamka ambako ni zaidi ya ufahamu wa Akili (au Zaidi ya maumbile).
Nilikuwa na shauku ya kuelewa kuhusu Uongozi wa Kiroho na ‟Intelligence” yao ambayo ilifanya yote yawezekane kwa njia ya Neema ‟Grace”. Hadi wakati huu mimi nilikuwa bado sijakuwa “Enlightened” lakini nilikuwa huru kuhusu siri ya kifo. Wakati natafakari kuhusu Ufunuo huu katika hofu na ajabu…. asubuhi moja Nilishuhudia Viongozi wangu wa kiroho ambao walikuwa wananisaidia niendelee na safari yangu ya ndani ya Nuru na Sauti.
Katika tahajudi hii ilikuja Sauti ya Kiroho ya juu, ambayo ilinichukua kwenye ngazi mbalimbali za ufahamu. Mara moja wakati huu Nilitambua nishati ya Sauti ni harakati katika ufahamu. Viongozi wa Kiroho walijitokeza kwangu kama mwanga wa duara unaowaka ambao unaweza kuwasiliana kwa ndani (si kwa njia ya kawaida) na pia kusafiri na ufahamu wangu wa kuniongoza mimi toka mzunguko mmoja hadi mwingine wa hali halisi. Viongozi hawa (Uongozi wa Viumbe wa Mwanga) walikuwa Watatu lakini kwenye masafa na Nishati tofauti.
Nilikuwa makini nika‟focus” na kuunganika na Kiongozi wa kwanza na kuvuka mzunguko wa Mwanga/ Sauti yake. Kisha nika‟focus” na kuunganika na Kiongozi wa pili. Mimi niliweza kuhisi uwiano, Umoja na kasi isiyo fikirika ya Nishati katika ngazi hii. Nilikuwa katika Ukweli mmoja wa Ufahamu wa Viongozi hawa wawili. Kiongozi wa tatu alikuwa (kwa lugha mtu wa kawaida) juu sana zaidi ya ufahamu wangu, na kadiri nilivyozidi kutahajudi, karibu zaidi, kwa kasi zaidi, uzoefu ulikuwa wa hila na kutoelezeki.
Nilimaliza kikao cha tahajudi hii na nilikuwa bado sijatatua siri ya Kiongozi wa Tatu wa Nuru ya Kiroho. Wakati nilipokaa kwenye kikao cha ‟Enlightenment” ndio wakati siri zote za kile nilichopitia kwenye ngazi hizi zilitatuliwa. Nilikaa kutahajudi kwa Uhuru wangu. Hakuna maneno ya kutosha kuelezea, lakini ngoja nijaribu kukuchukua wewe kwenye kile ambacho nilipitia.
Hakuna kitu kingeweweza kunitayarisha mimi kupokea zawadi hii. Ilikuwa ni wakati bora zaidi sana katika maisha yangu. Nilikaa chini na hisia ya haraka kama vile ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kukaa kutahajudi. Udadisi wangu wa ndani ulikuwa unawaka kwa ajili ya kutaka kutambua asili Yangu ya kweli. Niliomba toka ndani ya moyo kwa Viongozi hawa kunionyesha kuwa mimi ni nani. Nilitulia na kujiachia na kuachia kila kitu. Mwanzoni ilikuwa ni maono ya nyoka mwenye vichwa saba vya Dhahabu ambaye alikaa na mimi kwa karibu ya siku mbili. Hii ilikuwa ni ishara tofauti sana na ile ya ishara ya nyoka wawili wa Kundalini.
Hii inaonyesha ukamilifu katika ulimwengu wa juu wa ngazi za Kiroho. Wakati alama hii ilipotoweka nilitambua Mwanga na Sauti haviwezi kusafiri katika Vacuum (TUPU) na ni masafa ya mtikisiko unaoingia na kutoka kwenye Utupu. Wakati huu mimi mwenyewe nilijiuliza Safari iko wapi na vipi kuhusu Kiumbe wa Tatu wa Mwanga na masafa na uwianao amabao ulikuwa bado mipaka yake sijaivuka?
Baada ya kujiachia, siri zinaanza kujijibu zenyewe. Kulikuwa papo hapo Nishati ambazo hazikutoka Popote na kutoka Kila mahali kwa wakati mmoja. Ilinichukua toka Mwelekeo mmoja baada mwingine na kufikia ngazi hizi za Kiumbe huyu wa Nuru. Nilijiunga na masafa yake na ‟transcendence” ilitokea, kulikuwa na Mlipuko ya Mwanga Kila mahali! Hapakuwa na safari! Mwanga na Sauti zilifuata ufahamu wangu Kila mahali. Zilitoka kwenye huu Utulivu Kamili na kulikuwa hakuna siri tena!
Hapakuwa na hisia ya eneo na ni Uelewa mmoja. Kila mahali kwenye ngazi hii Nilijihisi mjinga, bila ya kujua chochote lakini Kuwa tu. Hata neno Kuwa bado lina maanisha Harakati. Ni ‟BE-NESS”! Niko huru. Mimi si Chochote. Hakuna mtikisiko wa nishati kama Mwanga na Sauti, katika Hali hii, ni mapumziko Kamili na Utulivu.
Viumbe watatu wa Mwanga wanawakilisha ‟Initiations” tatu. Hivi ndivyo mimi nilivyoshuhudia Uongozi wa Kiroho katika kazi na jinsi mimi nilivyofikia Lengo la maisha yangu.
Ninaandika haya kukuhamasisha wewe katika safari yako ya Kiroho kufunua Ukweli wa Kuwepo kwako. Hebu acha yote hii ifanye kazi katika Neema na Upendo bila masharti. Hebu tutumikie Lengo. WAKATI NI SASA. Chukua fursa hii na kutembea safari yako ya ‟Enlightenment” ili tuweze wote kusaidia ‟Ascension” ya dunia hii kwa kiwango cha juu kabisa iwezekanavyo. Pamoja na Neema ya Uongozi wa Kiroho yote haya yanawezekana sasa katika maisha haya. Napenda kwatakia heri wote katika Safari yenu ya Kiroho.