Ushuhuda (Y.F.)

 

Hadithi yangu inaweza kujaza vitabu kadhaa kuwaambia uzoefu wa maisha ya binadamu mdogo mwenye mipaka kama mtu mwingine yeyote. Ningesema maisha yangu hayakuwa rahisi, kama nikiongelea changamoto basi nilikuwa nazo kadhaa. Mara zote nimekuwa na nia kubwa ya Upendo, Ukweli na Uadilifu na nilitafuta haya yote katika sehemu nyingi ambazo si sahihi mpaka mahali pekee palipobakia kutafuta ilikuwa ndani yangu. Kamwe usiamini wewe hustahili Enlightenment au kwamba umefanya makosa mengi mno. Maisha yako yote yalikuwa ni wito wa kukuleta hapa ulipo. Niamini mimi, kama hamu yako na unachotaka ni Ukweli na Upendo wa Kweli, Njia hii ni kwa ajili yako. Enlightenment ni hatima ya binadamu wote. Sina nia ya kumkatisha mtu yeyote tamaa kwa kusema kwamba (Y) kamwe hukuwa Enlightened: mtu mdogo mwenye mipaka kamwe hawezi kuwa na uzoefu wa Kutokuwa na Mipaka (Limitlessness). Ndiyo maana natambua nini sio Mimi, na Mimi ni nini:

Mimi ni upendo. Mimi ni Ukiwa na Utupu, Mimi ni Kiini cha Kila kitu na Kila mtu. Niko kila mahali. Mimi ni Nuru inayoangaza Njia kurudi Kwangu. Mimi ni Sauti ambayo inakusafirisha wewe mahali ambapo ‟matter” haiwezi kufika, zaidi na zaidi ndani, kuvunja tabaka hadi tabaka ya mipaka mpaka kunifikia Mimi, Kiini chako. Pumzika Kwangu, Mimi ni Nafasi Tupu ambapo Maumbile yote yanadhihirishwa … Galaxies, Ngazi mbali mbali (Dimensions), Nyota, Sayari, Viumbe kutoka Kila Nyanja, Masters Waliopaa, Watu, Wanyama, Mimea, Bahari, Fire, Rains … Kila kitu kinakuongoza Kwangu. Sijawahi kamwe kuzaliwa, Mimi kamwe sitakufa. Wewe ni shahidi yangu. Chunguza kila kitu kinacho kuzunguka, kila kitu kinachotokea ndani na nje Yako. Kumbatia na kubali kila kitu na wewe utapumzika Kwangu. Kila kitu kinadhihirishwa ndani Yangu. Mimi ni UKweli, hakuna ukweli mpaka upumzike Kwangu.