Ushuhuda(O & C)

 

Sisi ni (O) na (C), tumekuwa Initiated kwenye tahajudi ya Mwanga na Sauti na tunataka kuwaeleza kuhusu uzoefu tulioupata leo.

Baada ya siku mbili za kutahajudi na baada ya kutembea porini tuliamua kukaa na kutahajudi, na baada ya kutahajudi tumehisi Upendo mkubwa kwenye mioyo yetu na tuliyeyuka pamoja na kumkumbatiana, tangu wakati huo mzunguko wa ‟vibration” zetu zimeongezeka kuwa maono safi ya Uzuri na Maelewano, mikono yetu ilivutwa kama sumaku tukiwa njiani tunarudi kwenye kituo cha faragha tulihisi haja ya kukumbatiana kila baada ya hatua 20 na mwezi kamili ukiangaza njia yetu. Kila mahali macho yetu yalipoweza kuona, maisha yalionekana kuwa hai zaidi: mimea, siafu na miti … kila kitu kilikuwa kizuri zaidi na mahiri.

Tuliingia chumbani kwenye kituo chetu na tukaamua kupumzika kwa dakika kumi kabla ya chakula cha jioni, tulishikana mikono na nguvu ilitokea, nguvu hii ilianza kupanda kwenye miili yetu hadi kufikia hatua ambayo hatukuwa na hisia ya mikono yetu wenyewe na muungano wa ‟matter” na nishati ulitokea. Kisha tuliamua kuungasha mikono mingine ili kuunda mzunguko wa nguvu, nishati ilianza kusonga na ku”squirm” na kuiweka tena miili yetu kwenye baridi, joto na mshtuko na hisia ya umeme, hata mikono yetu ilikuwa ”vibration” safi. Pia tulipata uzoefu jinsi ambavyo hii Vortex yote ya nguvu ilibadilishwa kuwa ukuta imara na ilianza kutembea taratibu vizuri na kuzunguka kama propela, nishati iliyotengenezwa ilipanda kwenye mikono yetu, na ikamfikia (O) kichwani na moyo wa (C). Sisi tulikuwa zaidi ya saa 2 tumeyeyuka pamoja, kuunganisha tukawa mmoja, tukiwa hatuna uwezo kusogeza mikono yetu na viganza vyetu kwani vilikuwa kitu kimoja tu.

Tunashukuru sana na furaha kwani sisi tunahisi hatimaye tulipata uzoefu wa nguvu ya Upendo (Universal Love). Sasa tunajua jinsi ya kubadilisha dunia, asante.