Kwa vile kuna Njia nyingi za kiroho zilizopo kwa Mtafutaji hasa, kuchagua mojawapo itakayoongoza kwenye Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho wa Kweli inaweza kuwa kazi ngumu.
Hii haisaidiwi hasa kwa ajili ya upungufu ya muda na eneo la Kijiografia.
Kwa hiyo inabidi kuwa waangalifu, kubagua na ujasiri.
Ni muhimu kwamba tunasoma, kwa makini, maandiko ya Njia na kuuliza maswali ya kupenya kwa Watahajudi wanaodai kuwa wametembea Njia hiyo. Ni bora kuuliza zaidi ya mtu mmoja na kuhakikisha kwamba ushahidi wao wote ni sambamba pamoja na mafundisho.
Watu wengi wanasoma maandishi na mafundisho yetu na kuyatathmini madai yetu. Jambo moja hasa linalonekana kuleta mashaka kwenye akili zao. Ni kasi ambayo baadhi ya Watahajudi wetu wanaeendelea kutoka ‟Initiation” ya Kwanza mpaka kupata ‟Enlightenment” (Hali Kamili ya Umoja).
Kiakili, wanalinganisha na Njia za jadi ambazo huchukua vipindi vingi vya miaka kumikumi na hata maisha mengi na kuhitimisha kuwa kile tunachokisema hakiwezi kuwa ‟Enlightenment” ya kweli. Hili ni hitimisho la busara. Hata hivyo, tunaishi katika wakati wa hali kali ya ambayo inahitaji hatua kali ili kurekebisha usawa ili kuleta amani na ustawi kwenye Sayari hii.
Kwa hiyo Njia ya kiroho tunayoisema sisi haiwezi kulinganishwa moja kwa moja na zile za zamani. Ni Njia ya leo (2016). Ni muhimu kuleta Nguvu ya Kiroho kwenye Sayari kwa njia ambayo kamwe haijawahi kuonekana, na kufukia lengo hili Watahajudi wengi wanahitaji kuendelea haraka kwenye Njia ili waweze kuwa na jukumu muhimu katika ukuaji wake. Tuna maana kwamba wanahitaji kufikia ‟Enlightenment” ili waweze kusaidia ‟Kuanshia” idadi kubwa ya watu ili kufikia mabadiliko yanayohitajika.
Suala jingine ambayo mara nyingi linajitokeza ni kwamba mtu anayetafuta na kutembea Njia ya kiroho anahitaji kushughulikia miili yao chini: ‟ego” zao, hisia na akili. Huu tena ni mchakato ambao, kijadi, unaweza kuchukua maisha yote. Hii pia ni hoja halali.
Tumeambiwa na Uongozi wa Kiroho kwamba Wao wanafahamu tatizo hili. Kwa sababu hiyo, wao wanatumia Nishati ya Kiroho ambayo hutumiwa na Watahajudi walioanzishwa ili kuleta mabadiliko katika ngazi ya kibinafsi. Kwa hiyo kadiri Mtahajudi anavyoendelea Kiroho, hupata mabadiliko sahihi ya miili yao ya chini, ili kuwawezesha kuelelezea Hali za juu za Upendo, Unyenyekevu na Huruma.
Uongozi wa Kiroho wana “picha kwa ujumla” na wanatumia kila kitu kwenye Uwezo wao ili kuleta mabadiliko muhimu yanayohitajika. Tunaambiwa kwamba ukuaji wa haraka na maendeleo kwenye Njia yataanza kupungua baada ya lengo letu la ‟Initiate” 75,000 kufikiwa. Kama ilivyoelezwa mahali pengine tunatarajia hili kupatikana katika kipindi cha miaka 3!
Kama una maswali yoyote kuhusu hii au makala yoyote, katika tovuti hii, tuandikie kwa kutumia Ukurasa wa Mawasiliano.