Ushuhuda (P.P.G.)

 

Kwa kawaida nimezoea kupata maumivu mengi wakati wa ‟period” hivi kwamba ni lazima kumeza dawa za kutuliza maumivu kila baada ya saa saba hadi nane kwa siku tatu za kwanza katika kipindi changu. Na kama nikichelewesha hata dakika chache, tumbo langu huuma sana, natapika na kuwa mgonjwa kweli, hata kutembea siwezi. Kawaida huchukua na kumeza dawa za kutuliza maumivu kuanzia siku ya kwanza na siku ya pili na wakati mwingine hadi siku ya tatu nikiwa kwenye ‟period”.
 

Wakati huu nilipoingia kwenye ‟period” nilianza kuhisi maumivu kama kawaida, lakini sikuwa dawa za kutuliza maumivu nyumbani, hivyo mimi nilikuwa karibu kutuma na kuagiza dawa za kutuliza maumivu. Lakini toka ndani yangu niliambiwa kuacha kutuma na kuagiza dawa za kutuliza maumivu na kuwa na TUMAINI! Mwanzoni haikuwa na maana kabisa, ilikuwa ni vigumu kuamini tu na kuwa na matumaini! Hii ni kwa sababu mimi najua jinsi ‟period” zangu zilivyo ngumu. Lakini nilihisi kama labda inanilazimu kujiachia na inanilazimu kuamini kile ninachoambiwa, na hivyo sikutuma na kuagiza dawa za kutuliza maumivu.
 

Nilikuwa nimelala chini kwenye kitanda nahisi maumivu, na nikaambiwa kufungua mikono yangu na viganja vyote vya mikono na kuelekeza juu. Nilifanya hivyo! Kisha nikaanza kusema “Mimi ni njia safi na napokea uponyaji”. Wakati mikono yangu bado ikiwa wazi na kuelekea juu, nilianza kutuma shukrani kwa Uongozi wa Kiroho na nafsi yangu ya juu na kuomba kuponya. Kisha nilichukua mikono yangu na kuiweka pamoja na kuanza kuisugua pamoja.
 

Kumbuka nilikuambia kuhusu jinsi ambavyo najisikia kwenye mikono na viganja vyangu? Kama kuna moto unachoma na kwamba hata wakati mwingine inabidi kuimwagia maji ili kuipoza! Hivyo wakati nikisugua mikono yangu pamoja, nahisi kama moto kabisa kwenye mikono yangu. Inakuwa ya moto sana.
 

Hivyo baada ya kusugua mikono yangu mpaka nikahisi kulikuwa na moto wa kutosha, mimi nilichukua mikono yangu na kuweka juu ya tumbo langu. Lakini niliambiwa kuiweka katika njia ambayo ingechora ishara. Niweke mkono yangu hivi kwamba kitovu changu kitakuwa katikati ya viganja vyote viwili. Vidole gumba viligusana na pia kwa upande mwingine vidole vya kwanza viligusana, na kujiunga na kufanya ishara ya sura ya almasi (kama alama) kwenye karata. Sijui hasa jinsi ya kuelezea umbo hili, lakini kwa namna fulani ni sawa na almasi kwenye kadi ya karata.
 

Hivyo niliendelea kupumzisha mikono yangu juu ya tumbo langu wakati ikiwa kama inachora ishara hii kwa muda, kama dakika moja hivi, kisha nikasugua tena mikono yangu na tena kuweka kwenye tumbo na kuchora ishara hii tena, na tena. Nilikuwa nafanya hivyo muda wote. Na wakati nafanya hivyo, niliendelea kusema “Mimi ni njia safi na mimi napokea uponyaji”.
 

Chini ya dakika tano, nilikuwa nasikia nafuu. Na chini ya dakika kumi tumbo langu liliacha kuuma kabisa. Sijameza dawa za kuzuia maumivu, na sasa ni siku yangu ya tatu ya ‟period”. Siku ya pili (jana), nilianza kujisikia maumivu kidogo, maumivu kidogo ya tumbo na mara nilifanya hatua za uponyaji, na mara maumivu yakatoweka. Huu ni wazimu ningesema kuwa sijui njia bora ya kuielezea. Lakini kutokumeza dawa za kutuliza maumivu wakati wa ‟period” yangu ni muujiza!
 

Baada ya kuongea na wewe jana usiku na kukueleza, uliniambia kukuandikia barua pepe, tulikuwa tunahama. Kufungasha na kuchukua vitu kwenda nyumba nyingine. Tulipokuwa njiani kurudi nyumbani, tumbo la Q. lilianza kuuma sana, sijui kwa nini. Alishuku kuwa labda ni kutokana na chakula alichokula. Sijui! Tulipofika nyumbani, alihisi uchungu sana kwenye tumbo lake. Tulitafuta dawa za kutuliza maumivu lakini hatukuweza kupata hata moja. Hapo nilikumbuka kuwa sikuziagiza siku nilipoanza ”period”. Na jana wakati tunarudi nyumbani tulikuwa tumechelewa sana na ilikuwa usiku na maduka yote yalikuwa yamefungwa. Tumbo lilikuwa linauma sana, na alikuwa na maumivu makali. Nilimuuliza kuwa nijaribu kumfanyia uponyaji ambao nilifundishwa kufanya! Alisema ndiyo kwani alikuwa kwenye maumivu makali. (Katika mawazo yangu nilikuwa nafikiri, “lakini huu uponyaji ni kwa ajili ya tumbo la ”period” tu. Hivyo kama nikimfanyia, je itamsaidia?” Nilikuwa najiuliza mwenyewe. Lakini nilidhani “kuna njia nyingine yoyote niliyonayo? Ni bora kujaribu “.
 

Ndipo nikainua mikono yangu juu, viganja vyangu vikiwa vinaelekea juu tena na kusema “Mimi ni njia safi na mimi napokea nguvu za kumponya dada yangu kutoa maumivu ya tumbo lake”. Pia nilimwambia aseme yeye ni njia halisi na yeye anapokea uponyaji. Kisha nikaanza kupeleka shukrani kwa Uongozi wa kiroho na nafsi yangu ya juu na kuomba uponyaji. Mimi nilichukua mikono yangu na kuanza kuisugua pamoja. Moto ulikuwa mkali sana nilihisi ulikuwa ukichoma mikono yangu. Kisha nikaweka mikono yangu juu ya tumbo la Q na kufanya ishara ileile juu ya tumbo lake. (Kitovu chake cha tumbo kilikuwa katikati, vidole gumba vyangu vilikuwa pamoja upande mmoja, na upande wa pili vidole vyangu vya kwanza vilikuwa vimeunganishwa pamoja).
 

Baada kama dakika tano alisema alikuwa anajisikia vizuri zaidi, na katika chini ya dakika kumi hakuwa na maumivu yoyote kabisa. Aliendelea kufanya shughuli zake kwenye simu yake. Mimi nilishangaa sana.
 

Hadi nilipokuwa nazungumza na wewe nilifikiri kile nilichopokea ilikuwa uponyaji tu kwa ajili ya maumivu ya tumbo la ”period”, lakini ilifanya kazi pia. Mara moja! Kweli ilishangaza!
 

Ninafikiria kwamba ni lazima kusambaza ujumbe huu kwa wengine, labda kama na wao wanaweza kufanya hivyo wakiwa na maumivu ya tumbo, au kama wakikutana na mtu mwenye maumivu ya tumbo au wanaosumbuliwa na maumivu ya tumbo la ”period”, inaweza kuwa msaada kwao pia.
 

Si rahisi kuelezea hii kwa maandishi lakini mimi nilijaribu kufanya hivyo kwa njia bora ambayo mimi naweza.