Watahajudi Maalum

 

Tunaambiwa na Uongozi wa Kiroho kwamba Nishati mpya ya ‟WimbiMwanga” (Lightwave) imeletwa na imeachiliwa kwenye Sayari yetu. Madhumuni yake ni kuruhusu idadi kubwa ya watu duniani kote wapate Kuanzishwa kwenye Mwanga na Sauti, baadhi yao watakuwa ‟Enlightened”. Hata hivyo kuna, sababu nyingine, ambayo inahusu kufikia kundi kubwa la Watahajudi 75,000 ambalo litakuwa na uwezo wa kubadilisha Ufahamu wa Sayari. Hii inafanyika kwa kutuma Upendo kwa njia ya mazoezi ya Kutahajudi.

Kadiri idadi yetu inavyokua, watu kutoka Dunia nzima na wa aina mbalimbali watajikuta wanavutiwa na lengo hili. Wao siyo lazima kuwa watajua ni kwa nini; wao watajisikia wanavutiwa tu kuwa kwenye kundi hili. Wengi hawatakuwa kamwe na uzoefu wa Kutahajudi au hata kusoma kitabu cha Kiroho. Wengi hawatakuwa na imani kuhusu Mungu au kuwa na dini. Hii ni sawa kabisa; kile tunachofanya hakitegemei mambo haya; inahitaji mtu kutamani Ukweli tu na kutaka kuwatumikia binadamu wenzeke na Sayari ambayo wote tunaishi.

Tumebaini tayari kuwa, idadi ya watu wamepokea ‟Initiation” ya Kwanza wanaonekana kuwa watahajudi wa asili. Wao mara moja wanaunganika na Nishati za Mwanga na Sauti (karibu kana kwamba walikuwa wamefanya hivyo kabla). Wameonyesha uwezo wa ajabu wa kusafiri kwenye ngazi za Ufahamu na kutembea Njia na kuwa na maendeleo kwa kasi ya ajabu.

Sisi tunahisi kuwa hawa watu maalum wamechukua miili kwa wakati huu ili kusaidia kazi hii na kuongoza ukuaji wake. Wengi huonyesha uwezo wa kuponya na huonyesha unyeti uliokithiri wakati wa kushughulikia watu walioko karibu yao. Ingawa ni wazi kuwa wao ni maalum wana tabia ambazo zinafanana za upole, Uaminifu na zaidi kuliko yote Unyenyekevu.

Baadhi yao wameonyesha kwamba wana mawasiliano na Uongozi wa Kiroho. Kwa kawaida hii ilianza mara kabla ya kujiunga na kikundi. Walihisi uwepo unaowafunika, mara nyingi wakati wanatahajudi au wakati wa vipindi vya utulivu, wakati mwingine katika ndoto. Wakati mwingine kulikuwa na mawasiliano ya maneno ambayo walipewa baadhi ya maelekezo maalum.

Tunaamini wengi wa watu hawa watakuwa muhimu sana kwenye kuenea kwa Njia hii; wametumwa Kufundisha, kuhamasisha na kutoa msukumo. Wanavyoendelea kwanye Njia kwa kasi kubwa watakuwa kwenye nafasi na uwezo wa kuweza Kuwaanzisha wale walioko pamoja nao. Hii ndio njia ambayo namba wetu itakua ili kuwa na uwezo wa kufikia lengo hili muhimu.

Kama unadhani yale yaliyoandikwa hapo juu yanaoana na wewe, kama unafikiri kwamba umekuwa na mawasiliano kutoka kwa Viumbe au “Uwepo” ambao unaonyesha Upendo Halisi basi tafadhali wasiliana nasi. Tuko hapa kukupokea wewe na kukusaidia kuelewa uzoefu wako na kukuonyesha Madhumuni ambayo bila shaka yatabadilisha maisha yako milele.