Ushuhuda (l.K.)

 

Nikifikiria juu ya maisha yangu …..Nilianza kuwa na wito wa ndani nikiwa na umri wa miaka 7, wakati, nilipojikuta najiangalia kwenye kioo, swali likanijia kwa nguvu MIMI NI NANI? na kusababisha woga kwangu. Na hapo mara moja nikakimbia toka kwenye kioo!
 

Kama mtoto Nilihisi ile hofu ya fumbo, hata hivyo sikuweza kujiamini na kumuuliza mtu yeyote maana ya uzoefu huo. Mimi nilijihisi kama zaidi ya toleo moja ya kile ambacho ni mimi…..kusambaza fununu kwa maisha mengine ya awali.
 

Tulikuwa na biblia ya zamani nyumbani na nilikuwa nafurahia kusoma habari za kinabii. Kwa hiyo, mimi nilikua na kujikuta kuwa na shauku zaidi katika masomo ya mafumbo kuliko masomo ya darasani. Shuleni katika maktaba nikajikuta nasoma zaidi kuhusu dini mbalimbali, na kwa kiasi kidogo masomo ya kawaida.
 

Nikiwa na umri wa miaka 18 nilijaribu yoga, na tayari nikawa nimebadilisha makanisa kutoka Katoliki kwenda Protestanti, Assemblies of God na kwa Mashahidi wa Yehova, pia nilikuwa Muislamu kwa muda. Nilijiuliza Mungu yuko wapi na kama yupo, kwa nini hakuna uhusiano wa moja kwa moja?
 

Kwa hiyo, nilithubutu kuwa yule ambaye atasikiliza na kujisalimisha kwa wema mkubwa kwa ajili ya wote. Moyoni nilijua kulikuwa na jibu la siri hii yote lakini kwa namna fulani ilinichenga na kunikwepa kwenye akili yangu. Nilipokuwa na umri wa miaka 20 rafiki yangu alinilielekeza kwenye darasa la Yoga na kutahajudi, ambayo niligundua ilikuwa kituo cha watahajudi wa Mwanga na Sauti. Katika kipindi cha mwaka nilianzishwa katika tahajudi ya Mwanga na Sauti na (N) na (M) waliokuwa wanaanzisha wakati huo na kueneza mambo ya Kiroho.
 

Baadaye niliondoka kwenye kundi hili kwa sababu kadhaa, hasa kuhusu uaminifu na uadilifu na nikaendelea na maisha yangu, lakini bado nikawa ninatahajudi kwenye Mwanga na Sauti.
 

Miaka kumi baadaye, mwisho wa 2015, Nilihisi nahitaji msaada kuweza kumaliza jitihada yangu ya kutafuta Enlightenment. Nilihisi shinikizo kubwa kutoka ndani ambayo sikuweza kuipinga. Hivyo niliamua kurejea kwenye Njia kwenye lile kundi ”Path” lakini kabla ya kumaliza mchakato mzima nikakutana na Lightwave kwenye ukurasa wa Facebook.
 

Mnamo Mwezi Aprili 2016 nilikuwa na wasiwasi na siamini, lakini nikawasiliana na (D) ambaye alieleza vizuri sana kuhusu Ujumbe huu mpya wa kufanya mambo ya Kiroho yaweze kupatikana kwa watu wote.
 

Baadaye, wakati wa Neema ya mwezi Mei mwaka 2016 nilipata Initiation ya Pili ambayo kwangu ilithibitisha uhalali wa Njia hii mpya. Nilitambua kuwa mimi ni zaidi ya Maumbo yote. Kwamba Maumbile yote ni muujiza wa Mungu, kama mchanganyiko wa nguvu zilizopangwa, ambayo hufanya vitu vilivyo hai na visivyo hai. Nilitambua kwamba kifo ni udanganyifu tu kwamba sisi tuna mipaka na tunakufa.
 

Sasa, nikiwa na msukumo zaidi kutokana na hofu na ajabu ya hii Hali Supa ya Ufahamu, Nililenga Tahajudi yangu nikiwa na tamaa kamili ya kuwatumikia binadamu wengine ili waweze kufikia Ukweli huo nilioupata.
 

Miezi minne baadaye niliambiwa nikae kwa Tahajudi ya Enlightenment! Kwa namna fulani nilipambana na wazo la Tahajudi ya Enlightenment kutokana na hali ya kiakili na mawazo yangu na nyuma. Nilipokea Upendo na msaada pamoja na msukumo na kuhamasishwa na (N), (D), (J) na (Y). Nilikaa Kutahajudi kwa siku 14. Mara muujiza ulitokea baada ya siku tisa za Tahajudi yangu! Niliona na kutambua kwamba vitu vyote vinadansi kwa mipigo wa moto wa siri, ambao hutengeneza Maumbile yote yanayoonekana na yasiyoonekana.
 

Viumbe wa Mwanga au Viongozi wa Kiroho ambao waliongozana nami kwenye safari yangu niliwapita mmoja mmoja na baadaye nilitambua kuwa hawa walikuwa Viumbe ambao wanafanya kazi kwenye mfululizo wa ngazi mbali mbali za Mwanga na Sauti. Wakati kasi ya Mwanga na Sauti ni ndogo kuliko nani na wapi ufahamu wako upo ……… hiyo ndio jinsi ‟transcendence” inavyotokea.
 

Nilitambua, bila shaka, kwamba hakuna kitu zaidi ya Uelewa wa Kuwa kwangu. Kuona na Kuwa kimsingi ni jambo moja na hakuna mahali pa kunipata. Badala yake, Mwanga na Sauti zimo katika Ukiwa wa Nafasi Kubwa ya Uelewa wangu. Hakuna mahali pa kwenda, hakuna Safari, hakuna kitu chochote zaidi unaweza kufanya kuliko kuiga Siri ya Asili yenyewe. Yote ni Upendo, naweza Kuwa tu.
 

Hakuna ushahidi unaohitajika kwenye Ngazi hizi au zaidi kwa Kuwa Wewe. Hakuna maelezo; akili haiwi Enlightened; unyenyekevu au ‟simplicity” ya Hali hii inachenga akili kabisa. Hebu maandiko haya yaweze kukuhamasisha wewe kwenye Safari yako ya Kiroho. Usisikilize na kuleta siasa, lenga mtazamo wako ndani yako na majibu yote yapo yanakusubiri kufunuka kupitia Kwako.
 

Kwa Neema inayotoka kwa Uungozi wa Kiroho utafika Nyumbani na kupata siri ya Kuwepo kwa kila kitu.
 

Shukrani za pekee kwa (N), (M), (D), (V), (J) na (Y) kwa kuwa karibu na kutoa msaada na faraja ilipohitajika zaidi njiani.
 

Kwa Upendo (IK)