Ushuhuda (K.R.)

 

Nilianza kutahajudi mwaka 2006 na safari yangu mwanzoni ilikuwa ya ajabu, Nilitahajudi sana na kupenda uzoefu mpya niliokuwa naugundua. Kwa bahati mbaya hali yangu ya maisha ilibadilika ghafla na kwa bahati mbaya, iliathiri tahajudi yangu. Sikuwa na furaha kwa miaka mingi baada ya matukio hayo mabaya kwenye maisha yangu na ilikuwa vigumu kuelekeza mtazamo wangu kwenye tahajudi yangu. Wakati huo nilipata Initiation yangu ya Pili, ambayo ilikuwa na uzoefu mgumu. Hata hivyo, mimi nilivumilia kwani tahajudi yangu ilikuwa chanzo cha nguvu kubwa na utulivu katika maisha yangu. Pia nilikuwa katika kutafuta majibu ambayo bado sikuwa nayo.
 
Baada ya miaka mingi maisha yangu yametulia na upendo wangu wa kutahajudi umekuwa na kuongezeka nguvu. Nafurahi nimevumilia na kupita wakati mgumu kwa sababu sasa duara limekamilika na mimi nimekamilika. Nimekuwa na uzoefu na ufunuo wa ajabu tangu nimepata Enlightenment yangu; Najisikia kila kitu sio kigumu ila ni rahisi tena. Kujitolea kwangu na uamuzi wangu umekuwa na manufaa. Niko kwenye nafasi ya utulivu, utulivu thabiti wa ndani na nguvu. Nina subira zaidi, upendo zaidi na najielewa zaidi na kuwaelewa wengine sina tabia ya kuwahukumu wengine katika maisha yangu. Nasubiri kwa hamu nini kingine tahajudi itaoniyesha, kwa kuwa huu ni mwanzo tu wa safari yangu mpya.