Sisi tulitaja kwenye ukurasa wa nyumbani idadi ya ‟Initiations” ambazo zilitarajiwa kwa miaka 3. Idadi ya 75,000 iliwasilishwa kwetu na Uongozi wa Kiroho.
Tumekuwa tukijadili jinsi ambavyo kuleta ‟Spirituality” kwenye Sayari yenu kwa kutumia ”Initiations” nyingi inaweza kuongeza Ufahamu kwa ujumla, wa wakazi. Hii basi husababisha ufahamu zaidi wa Sayari kwa ujumla, Upendo zaidi na Amani, na migogoro kupungua.
Kuna kiasi fulani cha kundi kubwa la watu ambao wanahitaji kuwa Wameanzishwa na Kutahajudi mara kwa mara kwenye Mwanga na Sauti, kurekebisha usawa, kutoka mambo yalivyo sasa. Tukipiga mahesabu ya idadi sasa hivi, tunahitaji miaka 3 zaidi ya Neema. Kutakuwa na wale ambao wataondoka, hili lazima kuzingatiwa.
Kwa kiwango cha ukuaji wa sasa, kama sisi wote tukifanya kazi kwa bidii na kushirikiana, hakuna sababu kwa nini tusiweze kufikia lengo hili.
Hatimaye Upendo Utashinda kwani ndio Asili ya Uumbaji Wenyewe!