Ushuhuda (C.B.)

 

Initiation yangu imesababisha nipige mbizi kwa kina kirefu kwenye Nuru na Sauti. Ilikuwa ni jambo la kushangaza kufanya tahajudi ndefu kwa urahisi bila shida pamoja na lengo jipya kwa ajili ya Ufahamu wangu. Sauti sasa iko pamoja nami muda wote kwa siku nzima. Ninahisi ni rahisi kuipata Nuru kwenye tahajudi. Mimi nina furaha kukubali baraka hizi na nina shukurani kubwa kwa kupata nafasi hii.