Ushuhuda (Y. F.)

 

Kadri mimi ninavyoweza kukumbuka, nilikuwa natafuta maana ya ndani katika kila kitu karibu yangu, nilikuwa nikitafuta ukweli wa ndani, nilikuwa na hamu ya upendo mkubwa, nilikuwa na ndoto ya kubadilisha ulimwengu kuwa mahali bora zaidi, hata mimi nikawa nimechoshwa na maisha mara nyingi nyakati ambapo imani ya haki na sio haki, mema na mabaya haikuweza kulingana na hisia kuwa yote yalikuwa sawa kwa namna fulani.

Roho yangu iliweza kukumbuka kumbukumbu ya maisha ya kupendeza ya ukamilifu ambayo moyo wangu, akili na mwili havijawahi kuwa na uzoefu huo katika maisha yangu yote.
Ni wakati tu ambapo niliangalia ndani yangu kwa njia ya kutahajudi niliona upendo, msamaha, kukubalika… Ni wakati tu ambapo niliacha kutafuta nikakumbuka, na wakati mimi sikukitarajia, wakati mimi nilijiruhusu tu mwenyewe kuwa… nilipata uzoefu wa utulivu wa kupendeza ambao maneno kamwe hayawezi kuelezea, katika hali ile ya utulivu mimi ni kila kitu na sio kitu kwa wakati mmoja… nilihisi kukumbatiwa na sauti ya ukimya…

Mimi ni mfereji (channel) tu, Ninashukuru kwa upendo usio na kikomo…

Tarehe 28 Desemba iliyopita ujumbe ulikuwa wazi, ulikuja kupitia kwenye ndoto na ikawa imechongwa kwenye roho yangu. Walisema:

“Tulitambua kuwa wakati mwingine unasahau kupumua kwa uangalifu na ufahamu kutoka mara moja hadi nyingine na hii inafanya wewe usahau wewe ni nani, na kuchukuliwa na kile ambacho wewe sio, tulikufanyia ” hivi ” wewe ili usiweze kusahau kuwa wewe uko hapa kwa ajili gani… Pumua kwa ufahamu…”

Ilikuwa ni rahisi na nguvu kwa wakati mmoja… Kati “Yao”, mimi nilitambua uso wa mtu mmoja ninayemjua kwenye dunia hii (physical plane), hivyo mimi mara moja niliamua kumwambia kuhusu ujumbe niliokuwa nimeupokea, kisha akanielekeza kwenye tovuti hii ya tahajudi ya Mwanga na Sauti. Ujumbe zaidi umekuwa unakuja tangu mfereji huu kufunguliwa. Ninahisi kama haina maana ya kutumia maneno ya kuelezea njia hii kuelekea kwenye Utambuzi wa Mungu, lakini natumaini inaweza kuhamasisha wengine.

Upendo wa Mungu uwe kwenu wote.