Wakati mtu anapoanzishwa kuna wigo wa uwezekano kuhusu kujiunganisha au ku“merge” kwao na Nguvu ya Mwanga na Sauti.
Itategemea mambo mengi ikiwa ni pamoja na: maandalizi, mawazo yake ya awali, uwezo wa kupumzika siku hiyo na woga wa kujiachia.
Maandalizi ni muhimu kwani mtahajudi atakaa kwa muda mrefu wakati wa siku ya Kuanzishwa, wakati mwingine hadi saa moja. Ni muhimu kwamba wanaweza kukaa kwa raha na makini na Nguvu bila ya kusumbuliwa na miili yao.
Mtafutaji anahitaji kuwa wazi. Kama wakienda kwenye Kuanzishwa wakiwa na mawazo ya jinsi itakavyokuwa au kama wana mawazo ya awali na uzoefu wa “kiroho”, haya yatakuwa pingamizi ya Ukweli. Ili kuwa na maendeleo kwenye njia yoyote msafiri anahitaji kwanza kuachia pale alipo! Tafadhali elewa kabisa kuwa hakuna imani inayohitajika, hiyo pia itakuwa kipingamizi cha njia. Njia bora ni kuwa na “canvas tupu” ambayo Nguvu zinaweza kuchora picha Zao.
Siku ya Kuazishwa mtahajudi atachukuliwa kupitia mfululizo wa mbinu za kutulia ambazo zinaweza kuhusisha pumzi na matumizi ya Mantra. Hii ni kumsaidia Mtafutaji kupumzika, kwani mvutano wowote ule utafanya Tahajudi yake ya Mwanga na Sauti, kuwa ngumu zaidi. Mvutano ni ishara ya kushikilia kitu fulani; Kutahajudi ni sanaa ya kuachia.
Wakati tunapoachia kile ambacho tunakifahamu na kuelekea kwenye kile ambacho hakijulikani ni jambo la kawaida kuogopa. Kila hatua katika Njia hii ni hatua ya kuelekea kwenye kile ambacho hakijulikani na kwa watu wengi wanaweza kuwa na wasiwasi. Kile kisichojulikana hakitupatii msaada au usalama; hapa ndipo Tumaini au ”Trust” inapohitajika. Wakati Nguvu Zinapofunuliwa Mtafutaji anahitaji kutambua kwamba Ni Muonekano mzuri tu wa Upendo usio na masharti. Hauwezi kukufanyia madhara yoyote; Ni Viongozi wako na Walimu waliopo kukuongoza na kuwa na wewe kwenda kwenye Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho ”Enlightenment”.
Hatimaye, hakuna Watahajudi kamilifu. Ni wazi kuwa baadhi ya watu ni bora kuliko wengine lakini sisi wote tunapambana kwa kiwango fulani. Hata hivyo, tukifanya mazoezi tunaweza kuboresha; tunaweza kuwa na lenga ”focus” kwa muda mrefu; tunaweza kuachia kwa urahisi zaidi
.