Ushuhuda (C.B.)

 

Awali nilikuwa nasita kuandika ushuhuda; hakuna mchanganyiko wowote ule wa maneno yoyote ambayo yanaweza kuelezea maana ya Enlightenment, sio wakati tu mimi nilipopata Enlightenment lakini hata sasa miezi miwili baadaye. Mimi bado kwa kiasi fulani ninasita, kwa hivyo tafadhali, acha niandike Msukumo badala yake.
 

Miaka mingi iliyopita wakati ndio kwanza nilikuwa naanza safari yangu ya kutahajudi, Adept alichukua muda wa kujadili na mimi. Ilikuwa kwa muda wa dakika chache lakini hizo dakika tano zilibadilisha maisha yangu.
 

Kuhusiana na safari iliyoko mbele yako alisema: “Kutakuwa na mambo mengi magumu na almasi nyingi”. Hayo maneno nayakumbuka hadi leo. Hilo, na Upendo alioonyesha kwa kuchagua na kupata muda wa kukaa pamoja nami na kunihamasisha. Hata katika ujinga wangu wa Kiroho, nilijua wakati huo, kwamba alikuwa anatokea mahali penye Upendo. Sikujua ule Upendo unaokumbatia kila kitu kwa jinsi ambavyo Najua sasa, lakini niligusa kiini chake, na alinigusa kwa namna ambayo haielezeki na kwa njia ambayo imenipa msukumo na kunihamasisha tangu wakati huo. Katika safari yote hii nimeshuhudia Upendo huu kutoka kwa Initiate wote na Adept kwa pamoja, na hii imenivutia zaidi kwa ajabu kwenye Safari ya Kiroho.
 

Baada ya kupata Enlightenment kwa mara ya kwanza, wazo langu sahihi kabisa lilikuwa: Sawa, ni jinsi gani naweza kuushusha huu UPENDO na kuwapatia watu wengine, chini kwenye kiwango cha vitendo ambayo hufanya kazi kwenye maisha yetu ya kila siku? Kile ambacho ni sehemu yangu na kinafikiri kilikuwa na tamaa kubwa ya kuelekeza huu Upendo Safi kwa namna fulani hivi kwamba kila mtu aweze kuuhisi.
 

Bado sina jibu kwa hili, zaidi ya mimi mwenyewe kuwa njia ya Upendo. Ni Upendo huu wa kila mtu na kila kitu ambao umesababisha mimi kukaa chini na kujaribu na kuweka baadhi ya maneno kwa matumaini ya kuwatia moyo na kuwahamasisha wengine kufikia UPENDO huu pia. Tafadhali, tafadhali kuendelea katika safari yako ya kufikia Enlightenment, nina uhakika itakuwa yenye thamani zaidi ya uwezekano wa wewe unavyoweza kufikiria. Sisi wote ni wadogo kwa nje, tuna mazuri na mabaya, hekaheka za, ajira, familia, hali mbaya, bahati mbaya, nyakati nzuri, furaha na majonzi, hayo ndio maisha. Lakini kumbuka, ndani sisi wote ni UPENDO – Upendo mkubwa – popote na kwenye hatua yoyote ile ya kutahajudi uliyopo. KUWA ule Upendo, ili ndani kuweze kuvuka ”transcend” nje. Uishi ule Upendo vizuri iwezekanavyo, hata kama ni kwa muda tu, na unaweza kumhamasisha mtu pia. Kila kitu huanza na Upendo.