Jitihada ya Amani

 

Kuna sababu gani ya Ku‟Initiate” na Ku‟Enlighten” watu wengi kiasi hiki?
Je, tunawezaje kuepuka nia za wale wanaorudia mara kwa mara kusababisha vita katika dunia hii?

Kutoka Uongozi wa Kiroho

Jibu lako halipo kwenye jinsi ya kuepuka (nia ya vita) lakini jinsi ya kubadilisha ufahamu wa dunia yenu. Mara tamaa ya madaraka inapogeuka kuwa uvamizi hakuna mengi yanayoweza kufanyika. Lengo letu tunalotaka kufanya hapa ni kwenda kwenye chanzo cha ‟psyche” ya binadamu na kujaribu kuondoa hii jitihada ya tamaa ya kuwa na nguvu na madaraka.

Siku zote kutakuwa na viongozi wa dunia ambao wanalazimika kufuata mahitaji ya wale wanaowatumikia. Tunachozungumza sisi ni umma na watu wa kawaida ambao wanachafuliwa na kile mnachokiita “Dunia ya Kisasa”, ambayo kwa wakati huu ina maana uvamizi mkubwa wa ‟Teknolojia Mpya” ambayo inaharibu mawazo ya watoto wenu ambao ndio watu wazima wa baadaye.

Nini basi kifanyike? Naam, katika ngazi ya Kiroho tunaweza kuongeza ufahamu lakini usije ukadharau nguvu ya taswira. Haichukui watu wengi kama unavyofikiria kuwa pamoja kama akili ya pamoja kuwazia maeneo yenye vita na hofu, chuki na tamaa ya madaraka na badala yake kuwa na upendo na msamaha.

Mawazo ya mtu binafsi yana nguvu sana: nini kitatokea ikiwa akili zenye nia moja zitaungana kwenye pambano la pamoja kwa ajili ya wema? Mnaweza kuanzisha harakati na kundi lenu la watahajudi.