“Aphorisms” za Phaedra

 

Tunao unyenyekevu mkubwa kwa kuwa na ‟aphorisms” 33 zilizoelekezwa kwetu kutoka kwa Uongozi toka kwa Mwanamke wa Mwanga anayeitwa Phaedra. Tumetoa orodha yake hapa chini na pia ni pamoja na ‟aphorisms” nyingine ambazo ni wazi upande wa kulia wa tovuti pamoja na ‟aphorisms” zingine. Ni matumaini yetu kuwa zitatoa msukumo ndani na nje ya tahajudi zako.

1. Baada ya kufikia lengo lako lingine daima litatokea. Kwa hiyo usifanye kitu kuwa lengo kama unatafuta ‟Enlightenment”.

2. Malengo ni adhabu kwenye uwanja wa maisha. Yanakuhadaa na kukughilibu kucheza mchezo.

3 Muda ni udanganyifu kuwa sisi tuko polepole mno.

4. Usitarajie chochote na Vyote vitafunuliwa.

5. Mwelekeo husababisha mgawanyiko: bila mwelekeo inaongoza kwenye ‟Enlightenment”.

6. Mto unapita lakini bado upo.

7. Hapo mwanzo kulikuwa na Neno: kabla ya mwanzo kulikuwa na Ukimya. Hapo mwanzo kulikuwa na Mwanga: kabla ya mwanzo kulikuwa na Giza.

8. Mtazamo wetu kikomo chake kinategemea uwezo wetu wa kuoana na Ukweli.

9. Kuwa katika mawazo kunatuweka duniani: kuwa nje ya mawazo kunatuweka mahali pengine.

10. Kuwa ndani ya mipaka huleta usalama: kuwa nje ya mipaka huleta Uhuru.

11. Usitoe ili uweze kupokea: Daima pokea ili uweze kutoa.

12. Ukimya hauwezi kupatikana kwenye sauti: lakini Sauti inaweza kupatikana kwenye Ukimya.

13. Giza haliwezi kupatikana kwenye mwanga, lakini mwanga unaweza kupatikana kwenye Giza.

14. Mwisho na mwanzo ni utenganikaji wa mawazo.

15. Tunapoangalia kwenye mwelekeo wowote mmoja tunakosa Kila kitu.

16. Sababu ni mwanzo tu wa kile kilicho.

17. Kile kilicho, kipo: kile kisichopo – ni Mungu.

18. Wakati maarifa yanatoa njia kwa kukubalika – Ukweli una nafasi.

19. Jibu linafunuliwa wazi wakati kuhoji kunaposimama.

20. Kujua ukweli ni kutojua: Kutojua kabisa ni Ukweli.

21. Mwishoni hakuna mwanzo: Mwanzoni hakuna mwisho.

22. Tunapoishi tunakufa: wakati tunakufa Tunaishi.

23. Kama ukiheshimu kila kitu karibu na wewe utagundua kwamba Kila kitu kinakuheshimu wewe.

24. Hebu nafsi iwe kweli na shukurani ili shukrani iweze kuifunua Nafsi.

25. Kioo huonyesha nafsi ikiangalia Nafsi na kisha inaonyesha kioo kuwa udanganyifu.

26. Utupu ni udanganyifu tu wa Uwezo.

27. Rangi hutokea wakati mwanga unayeyuka na melodi wakati Sauti inayeyuka… vyote ni vielelezo vizuri vya Umoja wa Milele.

28. Tunapotoweka tunakuwa Kila mahali.

29. roho ya Kiini ni kiini cha Roho.

30 Kama ilivyo Juu, ndivyo ilivyo chini: moja ni picha ya Nafsi, nyingine nafsi iliyojitokeza kama Umoja milele.

31. Muda hausubiri mtu yeyote; bali hatimaye hakuna mtu unayeweza kusubiri muda: Ni udanganyifu tu ambao tunatumia kupima mabadiliko.

32. Kadri tunavyosafiri mbali zaidi ndivyo tunavyoacha vitu vingi zaidi nyuma. Kwa hiyo tafuta mahali fulani ambapo haiwezekani kusafiri, hivi kwamba kusiwe na kitu tena cha kitapotea.

33. Wazo ni fremu moja kutoka kwenye filamu ya maisha. Usinaswe na kuishia kwenye mchezo tu: mtafute Mwandishi!