Jibu kutoka Uongozi wa Kiroho:
Mawimbi ni sehemu ya utaratibu wa maisha na nguvu zote zinaweza kuchukuliwa kuwa na wimbi kwa asili. Mawimbi pia yanakuja kutoka ngazi za juu, wakati dunia iko tayari, kuleta mabadiliko ya mageuzi. Hizi ni pamoja na “cheche” ambazo husababisha uvumbuzi mpya na teknolojia pamoja na mawazo mapya ambayo binadamu wanapewa wakati wamebadilika kwa kiwango fulani ili kuwa na uwezo wa kuyachukua mabadiliko haya.
Mzunguko ni muhimu kwa sababu ya asili ya Binadamu. Binadamu anahitaji muundo ili kuishi; lazima kuwe na utaratibu katika maisha ya watu. Kila siku jua linachomoza na kutua kwa muda wa kutabirika kama misimu inavyobadilika toka mmoja hadi mwingine. Mawimbi hupanda na kushuka kwa usahihi wa hisabati na wanawake kuonyesha mzunguko wa hedhi ambayo inahusiana na mwezi. Dunia kwa kuzunguka mara moja kwa siku, na kulizunguka Jua hufafanua mwaka na mara kwa mara mhimili wa Dunia kubadili mwelekeo wake. Hata tunavyopumua na mapigo ya moyo ni kwa rizimu ‟rhythmical”.
Haya yote huongeza utulivu wa Binadamu kukabiliana na heka heka za kuishi tu.