Pesa inaweza kuelezewa kama nishati. Inafanya mambo yatokee na inaruhusu watu kupata vitu vya kimwili. Pia inaweza kununua uzoefu na maarifa.
Thamani ya fedha ya kitu kwa ujumla hutokana na kile ambacho watu wako tayari kulipa. Hakuna chenye thamani kamili, inategemea bei ya soko ambayo daima hubadilika thamani.
Linapokuja suala la Elimu Ya Kiroho sisi tunaingia kwenye “minefield”. Kuna kiasi kikubwa cha habari, njia na mbinu ambazo zinauzwa ama kwa njia ya vitabu, video au mazungumzo. Mkusanyiko na tofauti ya bei inaweza kulinganishwa na bei ya magari: kutoka sifuri hadi mamilioni.
Na magari kwa ujumla ni rahisi kabisa kuona ni kwa nini gari linakuwa na bei fulani. Hata hivyo, kwenye Elimu Ya Kiroho haiwezekani kupima mambo yana thamani kiasi gani.
Linapokuja suala la bidhaa nyenzo unavyolipa zaidi ndivyo unavyotarajia bidhaa kuwa bora zaidi. Tunajua hii si kweli mara zote, lakini huwa hivyo mara nyingi zaidi. Ili mradi unatumia akili ya kidogo kwa ujumla utapata ulicholipia!
Kwa habari na mbinu mara nyingi uwiano ni kinyume: zaidi unavyolipa ndivyo kidogo unavyopata! Hii kwa kawaida hupatikana kwa njia ya ufungaji fujo (extravagant packaging). Kwa mfano majadiliano yanaweza kufanyika kwenye hoteli ya kipekee yenye ada kubwa sana ya kuingilia au maneno hayohayo yakasemwa bure kwenye kilima!
Kama kundi ilibidi kuamua namna ya kushughulikia suala la fedha. Kama tukitoza ada kubwa tutavutia idadi ndogo ya watu matajiri. Tungeweza tu kutoza ada ya kufidia gharama zetu lakini kulikuwa na uwezekano mwingine ambao unazingatia ukweli kwamba kile ambacho tunatoa kina thamani isiyokadirika.
Vilevile tulifahamu kuwa tunachotoa hakikuwa chetu na hatukuwa na haki ya kukiuza. Nguvu ambayo inatumwa wakati wa Initiation inatoka kwa Uongozi Wa Kiroho.
Watu ambao walikuwa wameanzishwa (Initiated) tu na kuguswa na Mwanga na Sauti Ya Mungu kweli wanajua thamani ya kile tunachotoa. Kwa kawaida wao ndio ambao watataka kutoa na kusaidia wanadamu wenzao. Kwa hiyo sisi tulianzisha mfumo unaotumia kanuni ya “Lipia Mbeleni”. Wale ambao waliopokea watakuwa ndio wanaweza kusaidia na kutoa kwa watu wapya.
Hii huhakikisha kwamba hakuna mtu au kikundi cha watu kitafaidika kifedha. Hatuna majengo ya kutunza na kudumisha na kama watu wanahitaji kusafiri basi wanapata wadhamini ambao hawajulikani. Hatuna fedha au akaunti ya benki na pia tunakataa michango.
Kama tukiangalia kati ya walimu wakubwa wa Kiroho ambao Ulimwengu umeona, yaani Buddha na Yesu, walitumia hasa mfumo huo!