Pale Elimu Ya Kiroho na Teknolojia Zinapokutana

 

 

Elimu Ya Kiroho na teknolojia sio maneno mawili ambayo mara nyingi unayaona pamoja, lakini yana uhusiano. Jarida la Brain World linaonyesha kwamba dini haikubali maoni ya sayansi kila wakati, lakini inachukua na kurekebisha moja ya matokeo mazuri ya sayansi: teknolojia. Kwa mfano, mwanzoni mwa karne ya ishirini, redio iliruhusu watu kusikia mahubiri ya kiinjili katika faraja ya nyumba zao. Televisheni, kwa upande mwingine, ilizaa wachungaji watangazaji wa televisheni. Wakati tuliongea juu ya hali ya kiroho na teknolojia katika ‘Chanzo cha Ujuzi wote’, tulisisitiza jinsi teknolojia inavyounda na kuongeza uwezekano wa kila mtu kugundua na kubadilishwa na hali ya kiroho. Kuleta habari chini na kuifanya iweze kupatikana kunaweza kusaidia watu kukuza maoni yao juu ya hali ya kiroho zaidi.

Halafu ukaja mtandao, ambao kiteknolojia ukawa badiliko kubwa kwa hali ya kiroho, kama vile ambavyo ilibadilisha jinsi watu wanavyowasiliana, kufanya kazi, na jinsi tunavyonunua vitu. Tovuti kama YouTube huruhusu waalimu wa kiroho kutangaza ujumbe wao bila kuhitaji kukusanya watazamaji. Kongamano la Mtandao Wazi (The Internet’s Open Forum) pia waliruhusu watu kushiriki katika majadiliano juu ya ibada zao na imani ya kiroho.

Yoga na tahajudi imebadilika na kuendelea kukidhi mahitaji ya ulimwengu kwa msaada wa vifaa vya kisasa. Dr Anil K. Rajvanshi anaamini hali ya kiroho ni kujielewa sisi wenyewe na sheria za ulimwengu kupitia zana za sayansi na teknolojia. “Ni hali muhimu inayotakiwa kwa maendeleo ya kiroho kwa kiwango kikubwa kuwa na maendeleo ya teknolojia,” aliandika. Teknolojia imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku na itakuwa muhimu zaidi kwa jinsi tunvavyoishi.

Utafiti mpya kutoka kwenye Chuo cha Tiba ya Perelman kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania uligundua kuwa 1.2% ya idadi ya wachunguzwa waliyohusika na vifaa vinavyofuatilia shughuli na vinavyoweza kuvaliwa. 80% ya watumiaji hawa walikaa na kifaa angalau kwa miezi sita. Watu wamevutiwa na ukweli kwamba wanaweza kujifunza zaidi juu ya jinsi walivyofanya wakati wa mazoezi kupitia data ambazo vifaa hivi huwasaidia kukusanya. Programu za kutahajudi pia huruhusu watumiaji kuona ni muda gani wamekuwa wakitahajudi kwa kutumia vifaa vya muda (timers). Hii inaongoza kwa watu zaidi na zaidi wanaounganisha maisha yao ya kiroho na teknolojia, ambayo kwa upande mwingine inaongoza kuwa na mahitaji ya programu zaidi ambayo inachanganya mambo haya mawili. Tathmini ya Chuo Kikuu cha Maryville juu ya tasnia ya programu inatabiri hitaji la wataalam milioni 1.1 ifikapo mwaka 2024, na teknolojia nyingi mpya zitakazotengenezwa zitaweza kusaidia watu kuungana vyema na hali zao za kiroho. Kutakuwa na vifaa vingi zaidi vitakavyotengenezwa ambavyo vinalenga kuboresha tahajudi na kusaidia watu kupata uhusiano mkubwa wa kiroho zaidi ndani yao.

Kwa mujibu wa mahitaji haya ya teknolojia ya kusaidia watu zaidi kujihusisha na hali zao za kiroho, Forbes anasema kuwa mashirika makubwa ya teknolojia kama Apple wanapaswa kufanya zaidi. Wanaamini kuwa yoga inapaswa kuwa mazoezi yanayofuatiliwa na kutekelezwa kwenye vifaa vyao vinavyoweza kuvaliwa kwani itawahimiza watu zaidi kujaribu zoezi hilo. Teknolojia ni jukwaa ambalo linaruhusu watu kuingiliana na mazoea mapya, iwe ya kiroho au sivyo, ambayo wasingeweza kufikiria kujaribu hapo awali.

Wakati zaidi yanaweza kufanyika, teknolojia inafanya maisha kuwa rahisi kwa watumiaji, inawaruhusu kuzingatia mambo mingine muhimu ya maisha yao kama familia na marafiki. Wakati huo huo, hali ya kiroho inatoa mtazamo fulani katika maisha. Wanapojiunga, watu wataweza kugundua vitu vingi vya kubadilisha maisha yao. Kwa mfano, maendeleo makubwa katika uwanja wa kiteknolojia inamaanisha fursa zaidi kwa watu kugundua sheria kubwa za maumbile na mwishowe Mungu.

Ujumbe uliyoandikwa na Reese Jones kwa ajili ya lightandsoundmeditation.com