Shukrani

 

Shukrani inaweza kujitokeza tu wakati fahamu zetu zimepanuka kiasi cha kutosha, ili kufunua na kudhihirisha mtazamo wa uhusiano kati ya binafsi na kile anbacho siyo binafsi.

Kisha tunaweza kuona udhaifu wetu, udogo na mipaka yetu, tofauti na ukubwa wa ulimwengu, ambapo tunakuta “kuwepo kwa uhai wetu”. Kwa kuonyesha na kuwa na shukrani, tunakubali kwetu wenyewe, na kwa wengine, hatari ya kiungo cha kuwepo kwetu.

Hii ni njia kamili ya kutangaza kukubalika, ambayo inatoa utupu wa kweli au nafasi, ambayo ukuaji halisi huanza.

Ukuaji mimi ninaosema hapa, sio ukuaji ambao mizizi yake iko kwenye vitu vya kimwili, lakini ukuaji halisi, ule wa Kiroho. Kwa kutahajudi kwa bidii, kwenye upeo wa juu kabisa wa Mwanga na Sauti, kadri binafsi ndogo inavyopanuka, itakuwa daima inayeyuka ndani ya Binafsi kubwa. Hatimaye, kwenye “Enlightenment”, tone la mvua litaungana kikamilifu na bahari ya ufahamu usio na mwisho, na udanganyifu wa kujitenga utapotea milele.

Cha kushangaza ni kwamba, wakati huu tunatambua kwamba shukrani tuliyokuwa nayo awali, ilikuwa kwa Binafsi yetu. Na, kujitokeza na kujionyesha kwa Nafsi kwenye maumbile, kumetoa ufunguo wa kufungua siri ya siri zote. Mimi ni nani?