Huduma, kwa wengi, itachukuliwa kama neno na dhana ya mtindo wa zamani. Katika dunia ya leo ya “mimi nitafaidikaje”, wazo la utii kwa njia ya kumhudumia mtu au jitihada fulani ni ya ajabu na kuonekana ya kizamani.
Hata hivyo, linapokuja suala la Kiroho, ni kitu tunapaswa wote kutafakari na kuidhinisha kama njia ya asili ya kutembea njia yetu. Kama tukiangalia Uongozi wa Kiroho wa viumbe walioko kwenye ngazi za juu za ufahamu, wao huonyesha kanuni hii ya Huduma daima na bila kuchoka. Kutokana na upendo wao mkubwa kupita kiasi kwa binadamu na aina nyingine ya maisha na viumbe vilivyodhihirishwa katika ulimwengu, wao hutumikia viumbe vyote, kwani hiyo ndiyo Chanzo na Asili yao.
Kwa hiyo, kama tukiwa na hekima tutajaribu kuakisi sifa hiyo katika yote tunayofanya. Mtu anapoanza kutembea Njia ya kiroho huwa ni kwa ajili ya, nini wanaweza kupata wao binafsi, lakini wataona kuwa mtazamo huu hautafungua uwezo wao wa kweli. Tatizo la kwanza wanalokutana nalo litakuwa tahajudi zao wenyewe: Kama wataelekea kwenye tahajudi zao kwa uchoyo na tamaa, hali za juu za ufahamu zitawakimbia. Hata hivyo, kama wakifungua mioyo yao ili kutumikia Nishati za Kiroho, hatimaye watapokea: hii inaonekana kuwa sheria ya Maumbile.
Ingawa tunaweza kutahajudi kila siku sehemu kubwa ya maisha yetu bado itakuwa katika ulimwengu, ambapo tutakutana na watu wengi, hivyo hapa ni mahali ambapo sisi tunajiandaa kwa ajili ya wakati wetu wa thamani kwenye mto (wakati tunatahajudi) na ni hapa hasa ambapo tunaweza kuhudumia. Tunaweza kujifunza kutoa bure na kwa uhuru kwa wale walio karibu yetu. Sio tu kwa ndugu zetu au marafiki lakini kwa wageni na watu ambao si lazima kuwa wanatuvutia. Wote wangefaidika kwa upendo na wema kidogo na kwa baadhi yao dakika chache za muda wetu zitakuwa na maana kubwa sana kwa maisha yao duniani.
Pili, lengo la Njia hii ni hatimaye kutumikai Viumbe wa Kiroho kwa kushusha chini Ufahamu na Hekima, ili kusaidia hii sayari yetu ambyo iko kwenye hali mbaya. Lakini kabla hawajaweza kutuamini kwa kazi hii wangependa “kuona” kwamba mioyo yetu ni safi na kwamba tuko nao sambamba na kuzingatia kwa ukamilifu matakwa yao, ili kufanya kazi hii kubwa.
Na hivyo ni dhana hii ya huduma ambayo ni ufunguo na muhimu kwa safari yako binafsi na safari ya wale wote utakaoweza kuwaleta kwenye njia hii, kwa kifupi kuhamasika na kufurahia na kushiriki kwa chanzo chake na wale walioko karibu na wewe. Kama itachukuliwa kwa upendo na unyenyekevu itaboresha maisha yako na maisha ya wengine zaidi ya vile unavyoamini. Pia ni huduma ambayo itaruhusu Uongozi wa Kiroho kuzungumza kupitia kwetu na kuokoa dunia yetu hii nzuri.
Huduma zaidi kuliko zote ni kuleta ya Roho kwenye ‟matter”.