Ushuhuda (D.P.)

 

Kutahajudi kwenye Mwanga na Sauti kumeongezea kina cha ajabu kwenye maisha yangu nikilinganisha na kitu kingine chochote kile nilichojaribu. Kwa miaka mingi nimeendelea kuyeyushia mbali zile sehemu zangu ambazo hazikuwa chochote zaidi ya kuwa vikwazo vya maendeleo yangu kwenye Safari yangu ya Kiroho na kuacha mimi kujihisi mwepesi zaidi, mwenye furaha zaidi na kuwa wazi zaidi kwa nguvu hizi za ajabu. Ingawa inaweza kuwa vigumu nyakati zingine, najua kutahajudi kwenye Mwanga na Sauti ni kitu muhimu na cha manufaa zaidi kuliko vyote ambacho naweza kufanya, na upendo wa ndani una lengo kuu la mwisho – kunionyesha kuwa mimi kweli ni nini!